MWENDESHA BODABODA AKUTWA AMEUAWA PORINIMadereva wa pikipiki maarufu bodaboda kwa kushirikiana na polisi katika Manispaa ya Mtwara Mikindani, wameupata mwili wa kijana Mohamed Juma (22) akiwa amefariki dunia katika pori la Kijiji cha Hiari, wilayani Mtwara.

Inadaiwa kuwa siku sita zilizopita, kijana huyo alikodishwa usafiri huo na watu wawili ambao hawajafahamika hadi sasa, wakitaka awapeleke kijijini hapo, na kijana huyo hakuonekana tena hadi mwili wake ulipokutwa leo porini humo ukiwa umefungwa kamba na ukiwa na majeraha.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments