BABA ADAIWA KUMPA UJAUZITO BINTI YAKE MWANAFUNZI


Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Tumaini wilayani Iramba mkoani Singida, amesimamishwa masomo baada ya kubainika kuwa na ujauzito anaodai kupewa na baba yake wa kambo, Abdallah Itambu anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 65 hadi 70.


Mwanafunzi huyo amesema ujauzito ulibainika baada ya uongozi wa shule kumpima katika Zahanati ya Kinampanda na kwamba baba huyo alikuwa akimlazimisha kufanya tendo hilo muda wa mchana na jioni ambao mama yake anakuwa shambani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post