'MHUNI' AKAMATWA KWA KUWEKA KAMERA ZA SIRI KWENYE MABAFU YA KUOGA WANAWAKE

Mfano wa kamera za siri
**
Mwanaume mmoja ameshtakiwa baada ya kamera za kadhaa za siri kupatikana katika vyumba vya wanawake vya kuoga katika ubalozi wa Australia jijini Bangkok nchini Thailand.


Wizara ya Australia ya Masuala ya Nje na Biashara imethibitisha kuwa polisi nchini Thailand walikamata mfanyakazi mmoja wa zamani mwezi jana.

Msemaji wa wizara hiyo alisema kuwa maslahi ya wafanyakazi wake ni suala la kipaumbele japo aligoma kuzungumza zaidi kuhusu mchakato wa kisheria unaoendelea kuhusu kisa hicho.

“Maslahi na ufaragha wa wafanyakazi wote ni kipaumbele kwa Wizara hii na tutandelea kutoa sapoti inayohitajika,” msemaji huyo alisema katika taarifa iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP.

Khemmarin Hassiri, kamanda wa polisi wa Thai wa masuala ya kigeni alisema kuwa ubalozi wa Australia ulikuwa umepiga ripoti dhidi ya mwanaume mmoja mnamo Januari 6 na kwamba uchunguzi ulikuwa unaendelea.

Haijulikani kamera hizo zimekuwa katika vyumba hivyo kwa muda gani lakini suala hilo lilitokea kujulikana bada ya kadi ya kamera kupatikana kwa sakafu ya vyumba hivyo kwa mujibu wa ripoti ya shirika la ABC Australia.

Kisa hicho kilidhihirisha ukiukaji mkubwa wa taratibu za usalama, mtaalam wa ulinzi na masuala ya kigeni ya Australia aliambai shirika la habari la AFP. “Kama usalama ulikuwa umedorora kiasi cha kuruhusu vifaa kama vile kamera kuweka mahali popote, inamaamisha kuwa ulinzi hata hautoshi kuuhakikishia ubalozi huo usalama wake,” alisema Hugh White, Profesa wa zamani katika Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Australia.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments