KONTENA LACHOMOKA NA KUUA MWENDESHA BODABODA DAR


MTU mmoja ambaye ni Mwendesha Bodaboda anasadikiwa kufariki dunia baada ya kuangukiwa na kontena lenye nafaka katika eneo la Tabata Bima, jijini Dar es Salaam.

Mtu huyo ambaye jina lake halijatambulika mara moja inaelezwa kuwa aliangukiwa na kontena lililokuwa kwenye lori baada ya lori hilo kukwepa daladala lililosimama ghafla na kontena kuchomoka.

Baadhi ya mashuhuda wamedai abiria aliyekuwa katika bodaboda hiyo alifanikiwa kuruka na kuikwepa ajali.

“Gari ya kontena ilikuwa inakuja kwenye njia yake lakini iliongozana na daladala, wote walikuwa spidi, ghafla daladala akasimama kuchukua abiria, dereva wa lori akalazimika kutanua kukwepa daladala ambapo kontena lilichomoka likaanza kuviringinga.

“Abiria wa bodaboda akaruka, lakini yule dereva akawa anahangaika namna ya kutafuta kukwepa ajali ile tayari kontena likawa limemfunika papo hapo,” wamesema mashuhuda wa tukio hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments