" ASKARI POLISI AKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA

ASKARI POLISI AKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA


Polisi wa kike kutoka nchini Jamaica, amekamatwa na dawa za kulevya aina ya Cocaine gramu 1,350 akiwa amezificha sehemu mbalimbali za mwili wake, wakati akijaribu kuingia nazo nchini Marekani.

Polisi huyo, Shelian Cherine Allen mwenye umri wa miaka 42, amekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Fort Lauderdale-Hollywood International Airport, muda mfupi baada ya kuwasili akitokea Montego Bay, Jamaica.

Kwa mujibu wa maafisa wa polisi, mwanamke huyo amekutwa na dawa hizo akiwa amezificha kwenye sehemu zake za siri, kwenye sidiria aliyokuwa amevaa huku pia akiwa amemeza takribani kete 90 tumboni mwake.

Endapo atakutwa na hatia, mwanamke huyo anaweza kuhukumiwa kifungo cha takribani miaka 40 jela.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments