WAZIMA MOTO AFRIKA KUSINI WADHIBITI MOTO ULIOUNGUZA MAJENGO YA BUNGE
Sunday, January 02, 2022
Ripoti kutoka Afrika Kusini zinasema kuwa kikosi cha zimamoto kimefanikiwa kudhibiti kwa kiasi fulani moto mkubwa uliokuwa ukiunguza jengo la Bunge la nchi hiyo jijini Cape Town.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kimataifa, moto huo ulianza lalfajiri ya leo Jumapili Januari 2, 2022.
Kikosi cha zimamoto kilikuwa bado kinaendelea kupambana na moto huo ambao chanzo chake bado hakijajulikana.
Hadi asubuhi ya leo, moshi ulikuwa bado ukifuka kutoka kwenye moja ya majengo kadhaa ya Bunge katika mji wa Cape Town.
Waziri wa Kazi za Umma na Miundombinu Patricia De Lille amewaambia waandishi wa habari kwamba hakuna ripoti za majeraha yoyote.
Vilevile Jean-Pierre Smith, mjumbe wa kamati ya Meya wa Cape Town inayohusika na ulinzi na usalama, amewaambia waandishi wa habari kuwa wazima moto wamegundua nyufa kwenye ukuta na paa moja lililoporomoka.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com
🚧🚦 Usiendeshe gari lako bila Mafunzo na Leseni halali_ 📲 Wasiliana nasi sasa: wa.me/255740273285 Unahitaji nini? 🚘 Unataka kujifunza udereva wa magari na kupata Cheti? 📄 Una cheti unataka kupata Leseni? 🔄 Unajua kuendesha lakini huna cheti wala leseni na unataka refresh upate cheti? 🛣️ Una nyaraka zote muhimu lakini unahitaji kujifua zaidi barabarani? ✅ Una Leseni bila cheti na unataka renew? 🌍 Tupo mikoa yote Tanzania hadi vijijini! 📞 Tupigie sasa: 0769 763 285
Social Plugin