RAIS SAMIA : VIJANA MSITUMIKE KUPASUA CHAMA
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan amewataka vijana wa chama cha Mapinduzi kutokubali kutumiwa kusababisha mpasuko ndani ya chama hicho.

Akizungumza wakati wa maandamano ya maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi y Zanzibar huko katika wilaya ya Mkoani Kusini Pemba leo Ijumaa, Januari 7, 2022 Rais Samia amesema kuwa vijana wote walio ndani ya cham a hicho wanapaswa kuwa mstari wa mbele kulinda na kusimamia ilani ya CCM.

“Vijana msitumiwe kukipasua chama, nendeni kakiimarisheni chama na jumuiya yenu. Vijana msitumike vibaya. Mapinduzi yaliyobaki ni Mapinduzi ya kimaendeleo, ni Mapinduzi ya kustawisha na kunawirisha Taifa letu, nendeni mkalisimamie hilo.


“Ukitenda vyema unajifanyia mwenyewe, na ukifanya mabaya unajifanyia mwenyewe, nendeni mkafanye mema tutakuoneni, mkianza kushiriki masuala ya rushwa na kupanga safu, mtajitia vidoti wenyewe. Viongozi wenzenu hao wamefanya mema mnawaona wameteuliwa huku na kule.

“Msitoe fursa kutumiwa kukipasua chama. Jeuri yenu, majidai yenu, kwenda kwenu kifua mbele ni kwa sababu chama kiko imara, niwatie moyo walezi wa Sasa hivi tunaoendelea kulea vijana, tusimame na vijana, tuwachunge, tuwalee katika maadili ya kitanzania.

“Uhai, usalama, maendeleo na ustawi wa Taifa lolote unategemea sana vijana, lakini hao ni vijana ambao wamelelewa vizuri, wamefunzwa itikadi na historia ya nchi yao, wakivikosa hivyo vyote fikiria itakuwa ni nchi ya namna gani,” amesema Rais Samia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post