NAIBU WAZIRI KIKWETE ATAKA WAMILIKI WA ARDHI KUJITOKEZA KUCHUKUA HATI


Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete akimkabidhi hati ya Ardhi Crispine Masero wakati wa ziara yake katika ofisi ya ardhi mkoa wa Dar es Salaam tarehe 17 Januari 2021.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete akiangalia ramani katika moja ya mbao za matangazo katika ofisi ya ardhi mkoa wa Dar es Salaam wakati wa ziara yake tarehe 17 Januari 2021.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete akiwasalimia wananchi aliowakuta ofisi ya ardhi mkoa wa mkoa wa Dar es Salaam wakati wa ziara yake katika mkoa huo tarehe 17 Januari 2021.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete akiangalia moja ya jalada la ardhi wakati wa ziara yake katika ofisi ya ardhi mkoa wa Dar es Salaam tarehe 17 Januari 2021.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete akiangalia moja ya jalada la ardhi katika Kituo cha Huduma kwa Wateja katika ofisi ya ardhi mkoa wa Dar es Salaam tarehe 17 Januari 2021.

***************************

Na Munir Shemweta, WANMM

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete amewataka wamiliki wa ardhi nchini ambao hati zao zimekamilika kujitokeza kuchukua hati zao ili waweze kupandisha tahamni ya ardhi wanayomiliki.

Kikwete alisema hayo tarehe 17 Januari 2021 jijini Dar es Salaam wakati akikagua Mfumo wa Unganishi wa Taarifa za Ardhi (ILMIS) akiwa katika moja ya ziara zake za kujifunza mambo mbalimbali ya wizara ya ardhi kufuatia kuteuliwa hivi karibuni kushika nafasi hiyo.

Alisema, kupatikana kwa hati kwa wale wamiliki wa ardhi kutarahisisha mambo mengi ikiwemo kupanda kwa thamani ya ardhi pamoja na kuitumia hati kwa kushughuli za maendeleo kama kuchukulia mkopo Benki.

Katika mkoa wa Dar es Salaam, kuna jumla ya Hati 3000 ambazo zimekamilika lakini wamiliki wake wameshindwa kwenda kuzichukua katika ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Dar es Salaam.

‘’Tumeshuhudia maeneo mengi hasa yale ya vijiji mtu ana eneo kubwa lakini eneo hilo linakosa thamani kutokana na kutokuwa na hati tofauti na Dar es Salaam mtu ana eneo dogo lenye ukubwa wa mita za mraba mia mbili au mia tatu lakini kutokana na kuwa na hati lina thamani kubwa’’ alisema Kikwete.

Katika kinachoopnekana kudhihirisha kuwa, Wizara ya Ardhi imedhamiria wananchi kupata hatimiliki za ardhi bila usumbufu na kwa wakati, Naibu Waziri wa Ardhi Ridhiwani Kikwete alimpigia simu mmoja wa wananchi wa Dar es Salaam aliyejitambulisha kwa jina la Crispin Masero ili aende kuchukua hati yake ambayo tayari imekamilika.

Ndani ya muda wa nusu saa mwananchi huyo aliweza kwenda ofisi za ardhi za mkoa wa Dar es Salaam na kukabidhiwa hati yake na Naibu Waziri Ridhiwani Kikwete ambapo aliipongeza Wizara ya Ardhi kwa kurahisisha huduma ikiwemo ya upataikanaji hati bila usumbufu.

‘’Kwa kweli niipongeze Wizara ya Ardhi pmaoja na wewe mhe Naibu Waziri naona umeanza kazi kwa kasi sana, asante sana’’ alisema Masero

Aliwataka wananchi waliopokea ujumbe wa kukamilika kwa hati zao kwenda katika ofisi ya ardhi kuchukua hati kwa kuwa wakichelewa wanaichelewesha serikali kupanga maendeleo.

Akielezsea mfumo wa Unganishi wa Taarifa za Ardhi (ILMIS), Naibu Waziri Kikwete alisema, mfumo huo ni kielelezo kuwa serikali imejipanga kutoa huduma za ardhi zilizo sahihi kwa muda mfupi na kwa gharama nafuu kwa wananachi wake.

‘’Mfumo huu unganishi unaongeza usalama wa miliki na kuboresha huduma zetu kwa wananchi, kama ambavyo nimeelezwa mfumo huu unaunganisha taarifa zote za umiliki kuanzia ngazi ya halmashauri na wizara na kjuwezesha utoaji hati za kielektroniki.

Hata hivyo, Kikwete alisema, bado ipo kazi ya kuboiresha zaidi mfumo huo wa utunzaji kumbukumbu za ardhi kwa lengo la kufikia kiwango kitakachowezesha baadhi ya hduma zinazotolewa ziwe zinaweza kuombwa na kujibiwa kwa njia ya mtnadao ili kupunguza msongamano.

Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Dar es Salaam Idrisa Kayera aliuelezea mfumo Unganishi wa Taarifa za Ardhi kuwa umerahisisha utendaji kazi wa haraka na wenye matokeo chanya katika sekta ya ardhi na kusisitiza kuwa hata makusanyo ya kodi ya pango la ardhi yameongezeka kutokana na mfumo huo..

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments