MSTAAFU WA JESHI LA POLISI AJIUA KWA WAYA WA PASI KISA MKE KAUZA KILA KITU AKIWA MGONJWA


MSTAAFU wa Jeshi la Polisi wilayani Mwanga mkoa wa Kilimanjaro bwana Omary Msangi amejinyonga hadi kufa bafuni kwake kwa kutumia waya wa pasi baada ya kwenda kutibiwa jijini Dares Salaam na aliporudi akakuta mkewe ameuza kila kitu ikiwemo nyumba na mashamba hivyo kulazimika kwenda kuanza maisha ya kupanga nyumba.

Tukio la kujinyonga mstaafu huyo limetokea usiku wa kuamkia jana akiwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi eneo la Kiboriloni Manispaa ya Moshi ambapo mwili wa mstaafu huyo ulichukuliwa na kupelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya KCMC.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio leo Jumatano Januari 26, 2022 akisema bado wanaendelea na uchunguzi wa kubaini chanzo cha kujinyonga kwa mstaafu huyo. “Ni kweli hili tukio limetokea na tunafuatilia kujua hasa chanzo cha kujinyonga kwake,” amesema Kamanda Maigwa.

Taarifa za chanzo cha kujinyonga kwa askari huyo kutoka kwa mmoja wa ndugu wa familia hiyo zinadai kuwa wakati mwanaume huyo akiwa kwenye matibabu mkoani Dar es salaam, mke wake alitumia nafasi hiyo kuuza mali zake zote ikiwa ni nyumba, mashamba pamoja na mali nyingine.

Inadaiwa kuwa baada ya mstaafu huyo kurejea nyumbani kutoka kwenye matibabu alikuta nyumba yake imeuzwa na kulazimika kwenda kupanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments