RAIS SAMIA ATANGAZA KUTEUA MAWAZIRI, WAKUU WA MIKOA WAPYA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema hivi karibuni atafanya mabadiliko ya viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Makatibu Wakuu na Wakuu wa Mikoa.

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumanne Januari 4,2022 Jijini Dar es salaama wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa fedha hizo kwenye miradi mbalimbali ikiwemo elimu, afya,maji na miundombinu.
Akizungumzia kuhusu mijadala inayoendelea juu ya serikali yake kukopa  kopa, Rais Samia amesema hizo kelele ni Presha 'Stres' za kuelekea uchaguzi mkuu 2025 hivyo ataweka pembeni ili wakutane mbele ya safari.

Amesema amewateua Wakuu wa Mikoa ili wamsaidie kuwaletea maendeleo wananchi.

"Wakuu wa mikoa nimekuwekeni nikiamini kule nilikowakasimia madaraka mtakwenda kusimamia kazi na wengine wote wakiwemo Makatibu Wakuu na Mawaziri",amesema.

"Nataka niwaambie nitatoa list mpya ya Mawaziri hivi karibuni, wale wanaotaka kwenda na mimi nitaenda nao ila wale wanaotumika nitawapa nafasi wakatumike huko nje wanapopataka. Wale ninaohisi wanaweza kwenda na mimi…nitakwenda nao. 

Lakini wale wote ninaohisi ndoto zao ni kule, na wanafanya kazi kwa ajili ya kule, nitawapa nafasi waende wakajitayarishe vizuri huko nje",amesema Rais Samia

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post