MAPACHA WAOA MAPACHA WENZAO WANAOFANANA

Wasanii maarufu ambao ni mapacha Tagwayen Asali kutoka Mji wa Kano Nigeria wame-make headline baada ya kufunga ndoa siku moja na wanawake mapacha wanaoitwa Hassana na Hussaina.

Unaambiwa mapacha hao wa kiume walikuwa wana ndoto ya kuoa mapacha wanaofanana ili wafunge nao ndoa na wanamshukuru Mungu kwa kujibu maombi yao.

“Kufunga ndoa na mapacha wanaofanana ni moja ya matakwa ambayo tumekuwa tukitafuta maisha yetu yote na Mungu uwe utukufu tumefanikisha hilo,” amesema mmoja wa mapacha hao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments