WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA MBOLEA CHA INTRACOM FERTILIZER LTD JIJINI DODOMA...'HUU NI UWEKEZAJI MKUBWA NCHINI'


Na Dotto Kwilasa-Malunde 1 blog, DODOMA.

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Kassim Majaliwa  ameridhishwa na ujenzi wa kiwanda cha mbolea cha Intracom Fertilizer Limited  ambacho  kitaajiri wafanyakazi 3,000 kitakapokamikika .

Kiwanda hicho kinajengwa na mwekezaji kutoka nchini Burundi kwa gharama ya  dola za Kimarekani milioni 180.

Hayo yamejiri leo katika  ziara yake ya kutembelea  ujenzi wa Kiwanda hicho kinachojengwa eneo la uwekezaji Nala Jijini Dodoma kinachotarajiwa kukamilika
baada ya miezi sita na kuanza  kuzalisha mbolea.

" Tunataka tulishe Afrika  Mashatiki, Nchi za Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Kusini mwa Afrika, (SADC ) Afrika nzima kuchukua chakula Tanzania tunaweza kuwa na hazina kubwa ya mahindi na mpunga" amesema.

Amesema lazima kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa uhakika wa mbolea ili wakulima wawe na uhakika wa uzalishaji.

"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alifanya ziara Burundi kwa lengo la kuboresha uwekezaji,zaidi ya dola milioni.450 zinatumika kwa ajili kuagiza mbolea nje ya Nchi,mkakati wa Rais ni kulinda fedha zibaki Nchini," amesema

"Huu ni uwekezaji mkubwa sana nchini kwetu,Kampuni hii ina kiwanda kingine Burundi,niliwahi kufika kwenye Kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha Tani 150,000 lakini kwa hapa Tanzania  kitazalisha tani 600,000, mahitaji ya mbolea ni makubwa tunataka kuimarisha sekta ya kilimo .," amesema.

Amesema  serikali itahakikisha mbolea yote inapatikana ndani ya nchi ili kuokoa fedha kiasi cha dola milioni 450 ambazo hutumika kwa ajili ya kuzalisha mbolea.

Pia ametaka kuwepo na mipango endelevu ya kujenga Barabara ya lami itakayofika eneo la Kiwanda hicho ili iweze kufikika kwa urahisi.

Licha ya hayo ametumia nafasi hiyo kuelekeza wizara husika kufanya utaratibu wa kuboresha miundombinu ya maji  Kiwandani  hapo na kueleza kuwa hali hiyo itaongeza tija ya uzalishaji wa mbolea.

"Watanzania wanaofanya  kazi ya ujenzi Kiwandani hapa mnapaswa kuwa na utayari wa kufanya kazi kwa bidii  ili kupunguza changamoto ya ajira Tanzania.

Kwa upande wake Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema mahitaji ya mbolea ni tani.700,000 na kiasi cha dola milioni 450 hutumika kuagiza mbolea nje ya nchi

Amesema mbolea itakayozalishwa Kiwandani hapo itakuwa na chokaa ili hutumika kutibu udongo ambao una asidi nyingi hali itakayopelekea kuongeza mazao.

Amesema sasa bei ya mbolea imepanda katika Soko la dunia ,mbolea aina ya DAP imekuwa ikiuzwa  dola 700 hadi 800 kutoka dola.400 huku mbolea ya Urea ikiwa  imepanda mara mbili .

Waziri Bashe amefafanua kuwa bei hizo zimekuwa zikilalamikiwa na wananchi lakini Serikali ina mikakati ya kumaliza changamoto hiyo na kueleza  mikakati inaendelea ya kuwekeza Kiwanda cha Urea mkoani Lindi.

Naye Waziri wa Mambo ya Ndani,Hamad Masauni amewahakilishia wawekezaji wote wanaokuja kuwekeza Tanzania  kuwa Tanzania ni salama na itaendelea kuwa salama.

Amesema Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia Idara ya Uhamiaji hawatakuwa kikwazo  kuhusu suala la vibali vya ukaazi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments