CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA LUSHOTO CHATOA MAFUNZO YA NAMNA BORA YA USULUHISHI WA MIGOGORO KWA MAAFISA WA EWURA


Mhe. Mohamed Chande Othman Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania akifungua mafunzo ya Kanuni na Mbinu za Usuluhishi wa Migogoro kwa maafisa    wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) hawapo pichani.

Mhe. Paul F. Kihwelo, Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto akiwakaribisha washiriki wa  mafunzo ya Kanuni na Mbinu za Usuluhishi wa Migogoro kwa maafisa    wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) hawapo pichani
Washiriki wa  mafunzo ya Kanuni na Mbinu za Usuluhishi wa Migogoro kutoka  Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wakiwa wanafuatilia  hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo kutoka kwa Mhe. Mohamed Chande Othman (hayupo pichani)
 Washiriki wa  mafunzo ya Kanuni na Mbinu za Usuluhishi wa Migogoro kutoka  Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wakiwa wanafuatilia  hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo kutoka kwa Mhe. Mohamed Chande Othman (hayupo pichani)
Mhe. Mohamed Chande Othman Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya  Kanuni na Mbinu za Usuluhishi wa Migogoro kutoka  Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).

***

Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania amefungua mafunzo ya Kanuni na Mbinu za Usuluhishi wa Migogoro kwa maafisa  kumi na tano  wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA). Mafunzo haya ya siku tano yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto yanafanyika   kuanzia tarehe 17 Januari mpaka 21 Januari 2022 Chuoni hapo.


Akifungua mafunzo hayo Mhe. Othman aliwaeleza washiriki wa mafunzo hayo kuwa mafunzo hayo ni fursa kwao kwani watabadilishana uzoefu kwa kuwa mafunzo hayo yamejumuisha washiriki enye taaluma mbalimbali na sio wanasheria peke yake.  Aliendelea kwa kusema kwamba kwa hapa nchini usuluhishi katika migogoro mingi haifanywi na wanasheria bali na wanataaluma wengine.


Kwa upande wake Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mhe. Dkt. Paul. Kihwelo ameeleza lengo kuu la mafunzo  hayo ni  kuwajengea uwezo maafisa hao wa namna ya kusuluhisha migogoro mbalimbali kati ya watoa huduma na wateja. Mkuu wa Chuo aliongeza kwamba mafunzo haya yatasaidia kuongeza ufanisi katika eneo hilo la usuluhishi wa migogoro.


“Tunaamini mafunzo yatasaidia sana kuwajengea uwezo na kuongeza ufanisi katika utendaji wao wa kazi wa kila siku”. Alisema Mhe. Dkt. Kihwelo.


Aidha, Mhe. Dkt. Kihwelo alieleza kuwa Chuo kina jukumu la kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya sheria ili kuwa na uwezo wa kusuluhisha migogoro mbalimbali inayotokea kwenye Mamlaka au Taasisi mbalimbali na kwa kufanya hivyo itapunguza mlundikano wa mashauri mahakamani.


Wakati huohuo Mjumbe wa Bodi na mshiriki wa mafunzo hayo,  Bw. Fadhili Manongi ameelezea kwamba mafunzo haya yatawasaidia sana katika utoaji wa maamuzi na kuweza kutenda haki pamoja na kutoa ushauri wa nini kifanyike kuhusiana na migogoro watakayokutana nayo.


Bw. Fadhili  ametoa ushauri kwa Mamlaka zote zinazofanya uthibiti, kuja Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kupata mafunzo kama haya.


Mafunzo hayo yamejumuisha maafisa wa EWURA wa ngazi mbalimbali ambao ni Wajumbe wa Bodi na wajumbe wa menejimenti.


Mada mbalimbali zitawasilishwa na wawezeshaji mahiri na wabobezi katika masuala ya mbinu za usuluhisi wa migogoro ambao ni Mhe. Mohamed Chande Othman Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Dkt. Paul Faustin Kihwelo Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mhe. Robert V. Makaramba Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mhe. Rose Teemba Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post