MTANGAZAJI MASHUHURI ZUHURA YUNUS ATANGAZA KUONDOKA BBC SWAHILI




MTANGAZAJI mashuhuri wa BBC Zuhura Yunus anaondoka kutoka shirika hilo baada ya kulitumikia kwa takriban miaka 14.

Zuhura atatangaza kipindi chake cha mwisho cha Dira ya Dunia leo Januari 14, 2022 majira ya saa tatu Afrika mashariki. Hata hivyo taarifa kutoka shirika hilo imeabinisha kuwa Zuhura amebakiza siku kadhaa za likizo kabla ya kuondoka rasmi.

Mtangazaji huyo aliyejiunga na BBC Swahili mwaka 2008 amesema anataka kuutumia muda wake sasa kuendelea na uandishi na mambo mengine nje ya BBC.


Taarifa ya Zuhura kuondoka BBC inakuja miezi kadhaa baada ya kuandika kitabu chake cha wasifu wa Biubwa Amour Zahor mwanaharakati mwanamke wa kisiasa wakati wa mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964.


Zuhura alianza kama mtangazaji wa redio na mzalishaji wa vipindi mwaka 2008. Mwaka 2014 alihamia Swahili TV na akawa mwanamke wa kwanza kutangaza Dira ya Dunia TV.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments