SPIKA NDUGAI : IPO SIKU HII NCHI ITAPIGWA MNADA




SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema kulingana na mwenendo wa Deni la Taifa kufikia Trilioni 70, ipo siku Nchi itapigwa mnada.

Amesema hayo wakati akizungumzia tozo zote za miamala ya Simu zilizopitishwa na Bunge akieleza zilipitishwa kwa lazima na mpaka sasa kuna majengo ya Madarasa na Vituo vya Afya vilivyojengwa kwa Fedha hizo.

Ndugai amesema tozo za miamala ya simu zilipitishwa ili nchi iweze kutekeleza miradi yenyewe, badala ya kutegemea mikopo ambayo imekuza deni la Taifa kufikia TZS trilioni 70. Amesisitiza haiwezekani miaka 60 baada ya uhuru nchi bado iwe ya kutembeza bakuli.

Ameitaka Serikali kuangalia namna mpya ya kupata mapato akiongeza, “Watu wengi wanatulaumu sana, ninyi ndio Wasomi. Hebu fikiria, Juzi mama kaenda kukopa 1.3 Trilioni deni.

“Na tuna majengo hivi sasa ya Madarasa, ya Vituo vya afya, ambayo yanajengwa kwa tozo. Hivi ipi bora? Sisi Watanzania wa miaka 60 ya Uhuru tuendelee kukopa na Madeni au tubanane banane hapa tujenge wenyewe bila madeni Makubwa yasiyoeleweka? Ni lini tutajenga wenyewe?

“Tutembeze bakuri ndo heshima? na tukishakopa tunapiga makofi! Sisi wa kukopa kila siku? Tukasema pitisha Tozo, anayetaka asiyetaka, pitisha Tozo. Lazima tuanze kujenga wenyewe. Nani atatufanyia? Yupo wapi huyo Mjomba? Tukapitisha Tozo.

“Sasa 2025 itaamua. Mkitoa waliopo sawa. Waje watakaokuwa kazi yao kwenda kukopa endepo hiyo ndo namna ya kuendesha nchi. Hivi sasa deni letu ni 70 Trilioni. Hivi ninyi si Wasomi? Is that healthy? Kuna siku nci itapigwa mnada hii. Madeni Madeni Madeni

“Bajeti yetu Trilioni 30, Trilioni 10 kati ya hizo kwa Mwaka tunalipa Madeni. Tumeenda Kukopa 1.3 Trilioni, Tunapiga Makofi. Tunawapa Wazungu Trilioni 10 Mariba Matupu. Wanatufanya Sisi Mazezeta.

“Hela yako Mwenyewe. Anachukua hela yako, halafu anakupa Kidogo Unashangilia. Toza fanya hivi, tujitegemee, Tusimame wenyewe. Kuna ubaya gani? Hata msomi anatupinga,” amesema Ndugai.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments