NAIBU KATIBU MPANJU:ASASI ZA KIRAIA NI MKONO WA KIUME WA SERIKALI MUNAFIKA TUSIPOWEZA KUFIKA.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju wakati akizungumza katika kikao kazi cha wadau wa masuala ya haki za binadamu kwenye Sekta ya Asasi za kiraia ambacho kimeratibiwa na Mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu (THRDC)
Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC ) Onesmo Olengurumwa akizungumza katika kikao kazi cha wadau wa masuala ya haki za binadamu kwenye Sekta ya Asasi za kiraia ambacho kimeratibiwa Mtandao huo.
Mwakilishi wa Kituo cha Sheria na haki za binadamu (LHRC) Raymond Paul akizungumza katika kikao kazi cha wadau wa masuala ya haki za binadamu kwenye Sekta ya Asasi za kiraia ambacho kimeratibiwa na Mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu (THRDC)

Wilbert Muchunguz Mwakilishi kutoka Taasisi ya Save the Children akizungumza katika kikao kazi cha wadau wa masuala ya haki za binadamu kwenye Sekta ya Asasi za kiraia ambacho kimeratibiwa na Mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu (THRDC)

Baadhi ya wadau wakiwemo waandishi wa habari walioshiriki  katika kikao kazi cha wadau wa masuala ya haki za binadamu kwenye Sekta ya Asasi za kiraia ambacho kimeratibiwa na Mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu (THRDC)

Picha ya Pamoja (picha zote na Mussa Khalid)

...................................

NA MUSSA KHALID,DAR ES SALAAM

Serikali imesema imekubali mapendekezo 108 ya mikataba ya Kimataifa ya haki za binadamu na itawasilisha taarifa ya nchi Februari 14 ,2022 na kuweka mfumo wa kushirikiana na Asasi za Kiraia.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju wakati akizungumza katika kikao kazi cha wadau wa masuala ya haki za binadamu kwenye Sekta ya Asasi za kiraia ambacho kimeratibiwa na Mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu kwa lengo la kupitia mapendekezo 252 yaliyotolewa  na nchi wanachama wa Baraza la Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu kwa Tanzania.

Mpanju amesema  mapendekeezo ambayo serikali imeyakubali ni ya hatua ya kwanza  hivyo mchakato huo utakamilika mwezi februari mwakani kwa kutoa taarifa waliyoyakubali na kuyakataa.

Amesema kwaniba ya Serikali wamerudi na mapendekezo kwa lengo ya kuyasambaza yote 252 kwa wadau serikali,taasisi na Mamlaka za Asasi za Kiraia ili kuyajadili na kupata mawazo  na ushauri kisha watapeleka kwenye kikao cha makatibu wakuu.

‘Sisi Wizara ya Katiba na Sheria tuko tayari kufanya kazi kwa karibu sana na nyie kwa sababu sisi sote na nia ya serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ni kuona watanzania wote wanazifikia haki na kunufaika nazo na haki kwa ujumla zinandelezwa kwa maslahi ya Tanzania na Makundi yote’amesema Mpanju

Awali akizungumza Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC ) Onesmo Olengurumwa amesema Tanzania imefanyiwa mapitio mara ya tatu ambapo 2011 ilikuwa ni mapitio ya kwanza na ilipata mapendekezo 153 na kukubali 107 na mwaka 2016 walipokea 227 na kukubali 133 sawa na asilimia 58 na kwa mwaka 2021 imeshuka kwa asilimia.

‘Ukiangalia mapendekezo mengi ambayo yamekataliwa kwa mfano Mapendekezo yanayohusiana na haki za kijamii ni mawili,kuhusu haki za wafugaji ni moja,kuhusu uhuru wa kujieleza ni 18,na mapendekezo yaliyokataliwa kuhusiana na haki za kiuchumi yalikataliwa na haki za wanawake na masuala ya jinsia 13 yamekataliwa na mapendekezo 9’amesema Mratibu wa THRDC Olengurumwa

Kwa upande wao wawakilishi wa mashiriki ya haki za binadamu,akiwemo Mwakilishi wa Kituo cha Sheria na haki za binadamu (LHRC) Raymond Paul pamoja na Wilbert Muchunguz kutoka Taasisi ya Save the Children wameipongeza Wizara kushughulikia mchakato huo utakaosaidia kufanya uboreshaji wa maswala ya haki za bianadamu.

Kikao hicho kimehudhuriwa na wadau mbalimbali wa masuala ya haki za binadamu kutoka maeneo tofauti nchini,wawakilishi kutoka Zanzibar pamoja na waratibu wa Kanda na wafanyakazi wa THRDC.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments