KATAMBI AFUNGA MWAKA 2021 KWA MKUTANO AKIANIKA MAMBO MAKUBWA JIMBO LA SHINYANGA MJINI

 

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ameendesha mkutano wa hadhara kwa kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi, pamoja na kueleza mambo ambayo ameyatekeleza ndani ya mwaka mmoja wa Ubunge wake.

Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, amefanya mkutano huo wa hadhara, katika mtaa wa Majengo Kata ya Kambarage, akiwa ameambatana na wataalam, Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Meya, pamoja na Kamati ya siasa ya CCM wilaya.

Akielezea mafanikio ambayo ameyafanya kwenye Sekta ya Afya, kuwa huduma zimeboresha kuwa karibu na wananchi, ikiwamo ujenzi wa Zahanati, vituo vya Afya, upatikanaji wa madawa pamoja na vifaa tiba.

Alisema pia katika Hospitali mpya ya Rufaa ambayo inajengwa katika eneo la Mwawaza, kunajengwa hospitali ya magonjwa ya mlipuko (Medical Tourism), ambayo itakuwa ikitibu magonjwa hayo ukiwamo ugonjwa wa UVIKO-19 ambapo kwa sasa ujenzi huo upo hatua ya msingi.

Kwa upande wa Sekta ya elimu, amesema alitoa kiasi cha fedha Sh.milioni 34.2 fedha za mfuko wa jimbo, kwa ajili ya kuunga mkono ujenzi wa vyumba vya Madarasa, ambayo yalianzishwa kwa nguvu za wananchi.

Pia, amesema miundombinu ya barabara imeboreshwa katika maeneo mengi ya Manispaa ya Shinyanga, yakiwamo yale ambayo ni korofi, pamoja na kujenga madaraja na makaravati.

"Sasa hivi ndugu zangu wana Shinyanga ni kipindi cha kazi tu na siyo porojo, na nitaendelea kuchapakazi kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali, kwa ajili ya kuwaletea maendeleo," alisema Katambi.

"Tumpongeza pia Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi, ikiwamo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, miundombinu ya barabara, madaraja, na vituo vya afya," aliongeza.

Aidha, alisema kwa upande wa ardhi, tayari wameshapata fedha Sh. bilioni moja, kwa ajili ya kupima, urasimishaji, na uthamini wa maeneo, ili wananchi wapate hatimiliki na kwenda kuzitumia katika mambo mbalimbali ya kiuchumi.

Katika hatua nyingine ,amezungumzia masuala ya kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo ukiwamo ujenzi wa stendi kuu ya mabasi, Soko, maegesho ya malori, na ujenzi wa chuo kikuu ambapo katika bajeti ya mwaka wa fedha ((2022-2023) miradi hiyo itaanza kutekelezwa.

Pia amehidi wananchi wa jimbo hilo, kuendelea kutatua changamoto zao mbalimbali, likiwamo suala la umeme, maji, barabara, katika maeneo ambayo bado yana changamoto hizo.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, pamoja na Meya wa Manispaa hiyo Elias Masumbuko, kwa nyakati tofauti wakizungumza kwenye mkutano huo, wameahidi kuendelea kushirikiana na Mbunge Katambi, kufanya kazi ya kuwaletea maendeleo wananchi.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara.
 
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge Katambi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge Katambi.
Diwani wa Kambarage Hassan Mwendapole, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge Katambi.

Chanzo - SHINYANGA PRESS CLUB BLOG

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments