Breaking

Post Top Ad

Sunday, December 26, 2021

KIJANA MATATANI TUHUMA ZA KUMUUA MAMA YAKE MZAZI KISHA KUTUMBUKIZA MWILI KWENYE SHIMO LA CHOO ARUSHA

Ruth Mmasi enzi za uhai wake

Jeshi la Polisi mkoani Arusha linamshikilia Patrick Mmasi (24) mkazi wa Njiro Kontena kwa tuhuma za kumuua mama yake mzazi, Ruth Mmasi (40) ambaye ni mfanyabiashara maarufu wa madini ambapo baada ya kufanya mauaji aliutumbukiza mwili katika shimo la choo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amesema wanamshikilia Patrick kwa tuhuma za mauaji  na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.

Inaelezwa kuwa  tukio limetokea Desemba 24,2021.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya familia hiyo, mmoja wa watoto wa marehemu Patricia Mmasi (19) anayesoma nchini China alipata mashaka akiwa China wakati alipojaribu kumpigia simu mama yake lakini haikupokelewa.

Amesema aliamua kuja Tanzania kwa ajili ya sherehe za Krismasi na alimuuliza Patrick kuhusu kutoonekaa kwa mama yake na kutopatikana kwenye simu ambapo ndugu yake huyo alimjibu kuwa mama yake akitoka huwa hamuagi na ndipo walipoamua kutoa taarifa polisi.

Amesema polisi walipofika walifanya upekuzi sehemu mbalimbali za nyumba hiyo ya kisasa ya ghorofa moja na ndipo wakabaini mwili huo ukiwa ndani ya chemba la choo nyuma ya nyumba hiyo na mwili huo umegundulika baada ya siku 14.

Ndugu huyo amedai marehemu alikuwa akiishi na kijana wake huyo ambaye ndiye mtoto wake wa kwanza na mara nyingi walikuwa wakitofautiana.

Mwili wa Ruth utazikwa nyumbani kwao kesho Jumatatu Desemba 27,2021 alasiri katika eneo la Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages