YANGA YAENDELEA KUGAWA DOZI...YAITWANGA RUVU SHOOTING 3- 1


Na Emmanuel Mbatilo - Dar es salaam

Timu ya Yanga imendelea kutoa dozi kwenye ligi ya NBC ambapo leo hii imecheza na Ruvu Shooting na kuichapa mabao 3-1 katika dimba la Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam

Ruvu Shooting ilianza kupata bao dakika ya 8 ya mchezo kupitia kwa nyota wao Rashid Juma.

Yanga iliwachukua dakika 32 kusawazisha bao likifungwa na Feisal Salumu "Fei toto" kwa shuti kali ambalo lilimshida kipa wa Ruvu Shooting Makaka na kuingia nyavuni.

Kipindi cha pili kilianza huku Yanga ikiendelea kutawala mchezo mara baada ya Ruvu Shooting kucheza pungufu baada ya nahodha wao Santos kupewa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu mbaya mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele.

Iliwachukua dakika 2 kipindi cha pili kupata bao mara baada ya mchezaji wa Ruvu Shooting kunawa mpira ndabi ya box na kuamuliwa penati ambayo ilipigwa na Djuma Shaban.

Bao la tatu la Yanga lilifungwa na Mukoko Tonombe mara baada ya kupewa basi tamu na Farid Mussa na kuachia shuti kali ambalo lilimshinda kipa na kuingia wavuni.

Yanga inaendelea kuongoza ligi kwa kucheza mechi tano na kujikusanyia pointi 15 huku akiruhusu bao moja tu katika michezo hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments