Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Amshukuru Rais Samia


Na Mwandishi Maalum, Dodoma

Mwanasheria  Mkuu wa Serikali (AG)  Dkt Eliezer Feleshi amemshukuru  Mhe.  Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa  kumuamini na kumteua katika nafasi ya  Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Dkt Feleshi ametoa shukrani hizo leo( Alhamisi)  Jijini   Dodoma, akisimama kwa  mara ya kwanza mbele ya   Bunge hilo  tangu alipoteuliwa kuwa AG na baada ya kula kuiapo cha uaminifu kwa Bunge hilo, wakati alipokuwa akiwasilisha  Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali ( Na 6) wa mwaka 2021 katika Mkutano wa Tano wa  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Napenda  kuchukua fursa hii kumshukuru sana Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania kwa kuniamini na  kuniteua  katika nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.” Akasema  AG Feleshi

 Na kuongeza “ Ninamuahidi kutekeleza  majukumu yangu haya mapya kwa weledi,  umahiri na uamininifu mkubwa”.

“Pili nimshukuru Mungu tena kwa kuniwezesha kusimama  kwa mara ya kwamba mbele ya  Bunge lako Tukufu kuwasilisha Muswada wa  Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ( Na 6) wa Mwaka 2021” akasema  Mhe. Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Akiwasilisha Muswada huo wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ( Na 6)  wa mwaka 2021 ( The Written Laws ( Miscelaneous Amendiments) No (6), Bill.2021, Mwanasheria  Mkuu wa Serikali amesema  Muswada huo unapendekeza marekebisho katika sheria  zifuatazao;

 Sheria ya  Kodi ya Mapato, Sura ya 332; Sheria ya  Usimamizi wa Kodi, Sura ya 438 na Sheria ya  Kodi la Ongezeko la Thamani, Sura ya 148.

Kwa mujibu wa AG Feleshi, Muswada aliouwalisha mbele ya Bunge, umegawanyika katika sehemu Nne ambapo sehemu ya kwanza ya Muswada inaainisha masharti ya  utagulizi, ikiwa ni pamoja na jina la Sheria pendekezwa na tamko la marekebisho ya sheria mbalimbali zinazokusudiwa kufanyiwa marekebisho kupitia  Muswada huo.

Akalieleza Bunge hilo kwamba,   sehemu ya pili ya Muswada huo inapendekeza marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Mapato, Sura ya  332, ambapo  kifungu cha 83B  kinapendekeza kufutwa kwa lengo la kuondoa kodi ya  zuio   ya asilimia mbili kwa mazao ya kilimo, uvuvi na ufugaji.

“Lengo la marekebisho ya haya ni  kulinda vipato vya wakulima kwa kuwapunguzia mzigo unaotokana na utozwaji wa kodi” amebainisha Dkt. Feleshi.

Kuhusu sehemu ya tatu ya Muswada, ikisomwa pamoja na Jedwali la marekebishoa ya  Serikali , inapendekeza marekebisho katika Sheria ya Usimamizi wa kodi Sura ya 438 ili kurekebisha kifungu cha 7 kwa  kuongeza kufungu kidogo cha 3.

“Marekebisho hayo  yanalenga kutambua Mkataba wa utekelezaji wa  Mradi wa Bomba la  kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda kwenda Chongoleani Tanga ili utekelezaji wa sheria  za kodi usiathiri masharti mahususi ya mkataba huo kama ilivyokubaliwa na pande zote

Kuhusu  sehemu ya Nne ya Muswada huo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema,  upande wa sehemu ya Nne ya  Muswada inayopendekeza marekebisho ya kufuta  sheria ya kodi ya ongezeko la thamani Sura ya 148, inapendeleza kufutwa. “ Hatua hiyo inatokana na  mashauriano ya  kina  kati ya  Serikali na Kamati

WAKATI HUO HU, Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Dkt. Feleshi, amewapongeza watumishi wote wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wakiongozwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt, Evaristo Longopa kwa kuendelea kutekeleza majukumu na  kazi za Ofisi  ya Mwanasheria  Mkuu wa Serikali, ikiwamo kuandaa Muswada huo na ambao umesimamiwa kwa karibu  na Bw, Onorius Njole, Mwandishi Mkuu  wa Sheria akishirikiana na Waandishi wa Sheria wa Ofisi ya Mwanasheria  Mkuu wa Serikali.

“ Tunatambua na tutaendelea kutekeleza  majukumu yetu kwa  weledi, ufanisi na  kuweka mbele maslahi ya nchi yetu” amesisitiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Feleshi.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments