KIJANA ATAFUNWA KIGANJA CHA MKONO NA FISI


Fisi

Emmanuel Ndete (20), mkazi wa Kata ya Kharumwa, wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita, amenusurika kifo baada ya kushambuliwa mpaka kukatwa kiganja cha mkono na Fisi, usiku wa Oktoba 29 majira ya saa 2:00 usiku wakati anarudi nyumbani kwake.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Geita Dokta Hiporitas Msimbe, amesema walimpokea mgonjwa huyo Oktoba 30, 2021, akitokea hospitali ya wilaya ya Nyang’hwale akiwa katika hali mbaya na kumpatia matibabu ambapo baada ya matibabu ya awali alipatiwa rufaa ya kwenda hospitali ya Bugando.

Itakumbukwa kuwa miezi saba iliyopita kikosi cha waganga wa jadi kutoka mkoani Shinyanga kilifanya operesheni maalum kwa ajili ya kumaliza Fisi hao ambapo walifanikiwa kuua Fisi zaidi ya 58 ambao walikuwa wakivamia na kupoteza maisha ya watoto kwa wakubwa na kupelekea watu kuishi kwa wasiwasi.

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments