Breaking

Post Top Ad

Thursday, November 11, 2021

SPIKA NDUGAI AWATAKA VIONGOZI WANAWAKE 'WASIVIMBE'


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai
***
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amewashauri wanawake viongozi kutotumia vyeo vyao vibaya bali wawe chachu ya kuaminika katika utendaji wao kwa wengine wanaowategemea.

Spika Ndugai ameyasema hayo Jijini Dodoma kwenye mafunzo ya uongozi kwa wanawake viongozi na wanasiasa ambapo amesema kama kundi la wanawake wakipewa mamlaka halafu wakaanza kuvimba na kushurutisha wengine kwa kuwaweka watu ndani basi ni wazi kunawaondolea sifa ya kuwa viongozi.

Kwa upande wake Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema wao wakiwa ni miongoni mwa wanawake wachache waliobahatika kupata nafasi za juu za uongozi wanahakikisha kufanya vizuri zaidi ili kubadili fikra mbaya za baadhi ya watu kuhusu wanawake viongozi.

Via EATV

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages