MWALIMU AKAMATWA KWA UDANGANYIFU MTIHANI WA DARASA LA NNE....KACHUKUA WA DARASA LA 6 WAFANYE

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Kamishna Msaidizi wa Polisi Shadrack Masiji akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake.

Na Costantine Mathias-  Bariadi.

JESHI la Polisi Mkoani Simiyu linamshikilia Mwalimu wa Shule ya Msingi Shimbale iliyoko Halmashauri wa mji wa Bariadi mkoani humo kwa tuhuma za kufanya udanganyifu kwenye mtihani wa darasa la nne uliofanyika Oktoba 28 na 29 mwaka huu.


Akizungumza na waandishi wa Habari, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Simiyu Kamshina Msaidizi wa Polisi Shadrack Masiji amesema mwalimu huyo alifanya udanganyifu katika mitihani ya darasa la nne kwa kuwachukua wanafunzi wa darasa la tano na la sita kwa ajili ya kuwafanyia mtihani wanafunzi wa darasa la nne ambao ni watoro.


"Jeshi la Polisi linamshikilia mwalimu wa Shule ya Msingi Shimbale aitwaye Gaudensia Onyango, (45) mkazi wa mtaa wa Shimbale kwa tuhuma za kufanya udanganyifu katika mitihani ya darasa la nne kwa kuwachukua wanafunzi wa darasa la tano na Sita kwa ajili ya kuwafanyia mitihani wanafunzi wenzao wa darasa la nne 23 ambao ni watoro", amesema Kamanda Masiji.

Ameeleza kuwa Wasimamizi wa mithani waliwakamata wanafunzi hao katika mitihani ya Hisabati na Kiswahili majira ya saa 5 : 00 asubuhi, siku ya Alhamisi Oktoba 28,2021.


Amefafanua wanafunzi wa darasa la nne hutumia kadi za maendeleo kwa ajili ya usajili na ukaguzi wakati wa mitihani, hivyo mwalimu huyo alikuwa akitoa picha za wanafunzi watoro na kuweka picha za wanafunzi wa madarasa ya juu ili waweze kufaulu.


Amesema serikali kupitia Wizara ya elimu kwa kushirikiana na Tamisemi wamekuwa wakitoa zawadi kwa shule zinazofanya vizuri, hivyo lengo la mwalimu huyo lilikuwa ni shule yake kupata ufaulu mzuri ili waweze kupata zawadi na kuwa kwenye nafasi nzuri kimatokeo.


Ameongeza kuwa hadi sasa mtuhumiwa huyo yupo mahabusu na anaendelea kuhojiwa kuhusiana na tuhuma hizo, na kwamba mara baada ya upelelezi huo kukamilika jalada litafikishwa ofisi ya taifa ya takwimu kwa mashtaka na hatua za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani.


Masiji amewataka watumishi wote wanaohusika na zoezi la usimamizi wa mitihani wa kidato cha pili na kidato cha nne kuacha mara moja vitendo vyovyote vya udanganyifu wa mithani kwani kamati za mithani ya wilaya na mkoa kwa kushirikiana na jeshi la polisi halitafumbia macho suala ya udanganyifu katika mitihani hiyo.


Ili kuwa wa Kwanza kusoma habari na matukio tunakushauri upakue/ download Aplikesheni ya Malunde 1 blog ili tukutumie moja kwa moja kwenye simu yako
Pakua App ya Malunde 1 blog,

 Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments