MKUU WA WILAYA AMWAMURU DEREVA WAKE ALIPE FIDIA AJALI YA KUUA KIFARANGA


Mkuu wa Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, Paul Chacha amelazimika kusimamisha Msafara baada ya Dereva wake Alfred Chaki kugonga Kifaranga cha kuku katika Kijiji cha Makingi alipokuwa anaendelea na ziara ya ukaguzi wa miradi ya mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko-19.

Mkuu huyo wa Wilaya alimuamuru dereva wake alipe fidia ya Shilingi “Elfu Tano” na alikemea tabia ya Madereva kugonga Kuku, Bata, Kanga au Mnyama wa aina yeyote na kisha kuondoka.

 Aidha, alisisitiza wananchi walime na kufuga kisasa ili wajikwamue kiuchumi.

Mkuu wa Wilaya Chacha pia aliwaomba radhi akina Mama waliokuwa eneo la tukio na walimshukuru na kumpa baraka za kuendelea na Safari.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments