TCU YATANGAZA ORODHA YA WAOMBAJI WALIODAHILIWA ZAIDI YA CHUO KIMOJA KATIKA AWAMU YA NNE NA WALE AMBAO HAWAKUJITHIBITISHA AWAMU ZILIZOPITA


Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inapenda kufahamisha umma na wadau wa Elimu ya Juu nchini kuwa Awamu ya Nne na ya mwisho ya Udahili kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza katika Taasisi za Elimu ya Juu nchini kwa mwaka wa masomo 2021/2022 umekamilika.
 

WAOMBAJI WALIODAHILIWA KATIKA CHUO ZAIDI YA KIMOJA 

Waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja katika Awamu ya Nne na wale ambao hawakuweza kuthibitisha udahili katika awamu zilizopita wanasisitizwa kuthibitisha udahili wao katika chuo kimojawapo kuanzia tarehe 24 Oktoba hadi 6 Novemba, 2021 kwa kutumia namba maalum ya siri iliyotumwa kwa ujumbe mfupi kupitia namba zao za simu au barua pepe walizotumia wakati wa kuomba udahili. 

Wale ambao hawatapata kwa wakati ujumbe huo, wanashauriwa kuingia kwenye mifumo ya udahili ya vyuo walivyodahiliwa na kuomba kutumiwa ujumbe mfupi wenye namba maalum ya siri iii kuweza kujithibitisha katika chuo husika. Aidha, uthibitisho wa udahili ufanyike kupitia akaunti ambayo muombaji alitumia wakati wa kuomba udahili.

Kuona Orodha ya majina ya waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja katika Awamu ya Nne na wale ambao walishindwa kuthibitisha udahili katika awamu zilizopita imewekwa katika tovuti ya TCU  


Orodha ya waombaji waliodahiliwa zaidi ya chuo kimoja au programu zaidi ya moja katika awamu ya Nne ya Udahili  na wale ambao hawakujithibitisha  awamu  zilizopita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments