SERIKALI YAIPONGEZA SUA KWA TAFITI ZA KILIMO ZENYE TIJA NCHINI

Mkurugenziwa Sera na MipangoWizarayaKilimo  Bwana Obadiah Nyagiro akiwasilisha hotuba yake kwa wadau wa APRA

Mtafiti kutokakatikaChuo Kikuu Cha Sokoine cha KilimoSUA  Profesa John Jeckonia akitoa ufafanuzi kwa wanahabari kuhusiana na matokeo ya utafiti huo.
Mkuu wa Mradi wa APRA na Mtafiti kutoka Chuo Kikuu Cha Sokoine cha Kilimo SUA  Profesa Aida Isinika akiwasilisha matokeo ya tafiti kwa wadau.
Mtafiti kutoka Chuo Kikuu Cha Sokoine cha Kilimo SUA Profesa Mtengua Mdoeakichangia jambo kwenye kikao hicho.
Dk. Christopher Magomba Mhadhiri na Mtafiti katika mradi huo kutoka Chuo Kikuu Cha Sokoine cha Kilimo SUA  akitoa maelekezo mafupi kuhusiana na tafiti.

Wadau wakifatilia wasilisho la matokeo ya Utafiti wa APRA.

Wadau wakifatilia wasilisho la matokeo ya Utafiti wa APRA.
Wadau wakifatilia wasilisho la matokeo ya Utafiti wa APRA.
Wadau wakifatilia wasilisho la matokeo ya Utafiti wa APRA.
Wadau wakifatilia wasilisho la matokeo ya Utafiti wa APRA.
Wadau wakifatilia wasilisho la matokeo ya Utafiti wa APRA.
Wadau wakifatilia wasilisho la matokeo ya Utafiti wa APRA.
Wadau wakifatilia wasilisho la matokeo ya Utafiti wa APRA.
Wasilisho likitolewa 
Wasilisho likitolewa 
Wadau wakifatilia wasilisho la matokeo ya Utafiti wa APRA.



Na Amina Hezron - Dodoma                                               

SERIKALI kupitia Wizara ya Kilimo imekishukuru Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa jitihadakubwa ambazo watafiti wake wanazifanya katika kufanya tafiti mbalimbali zenye tija za kilimo zikiwa na lengo la kusaidia kuboresha kilimo, kuinua maisha ya watanzania na kuinua pato la taifa.

Akizungumza  kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu waWizara ya Kilimo, Mkurugenzi wa Sera na MipangoWizara  ya Kilimo, Obadiah Nyagiro katika Warsha ya Kitaifa ya kutoa mrejesho wamatokeo yautafiti Mradi wa Utafiti wa Sera za Kilimo BaraniAfrika (APRA) liyofanyika leo mkoani Dodoma  amepongeza kazi kubwa iliyofanywa na watafitikwenye mradi huo na hasa kitendo chao cha kuamuakurudisha matokeo ya utafiti wao walengwa.

“Bila Utafiti hakuna jambo jipya lenye maamuzi yakiserikali linaweza kutokea, kama kuna matamkoyametoka bila utafiti utekelezaji wake hauwezi ukazaa mambo ambayo ni sahihi ambayo yanaweza yakaletamaendeleo kwa Wananchi, hivyo ni vizuri tafitizifanyike na mabadiliko ya sera yafanyike kulinganana uchambuzi uliofanyika” alisema Nyagiro.

Aidha Nyagiro ameeleza kuwa mipango yaSerikali hivi sasa inahimiza  kilimo cha alizeti nchiniili kupunguza uhaba wa upatikanaji wa mafuta ya kulana kwa mwaka huu wa Serikali   imedhamiria kusisitiza kuongeza Kilimo cha alizeti katika mikoa yaDodoma na Singida na inaongeza   bajeti ya utafiti kwaTaasisi ya Utafiti wa Kilimo(TARI) na kuwezeshawakala wa mbegu nchini ( ASA) ili  kusaidia mbegubora za alizeti zinapatikana kwa wingi.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo wa Sera naMipango Wizara  ya Kilimo alisema zao la mpungani muhimu kwa usalama wa chakula hivyo Serikali inahimiza 
sekta binafsi kushirikiana na serikali kuwekeza katika miundombinu ya umwagiliaji ili uzalishaji wa mpunga ufanyike angalau mara mbili kwa mwaka.

Akielezea matokeo ya tafiti hizo Mtafiti wa Utafiti huo kutoka (SUA) Prof John Jeckonia alisema kuwamatokeo makubwa ambayo tafiti imebaini kuwa kilimocha  

alizeti kimeleta mchango mkubwa katikakupunguza umasikini kwa kuongeza vipato vya watu.

Alisema fursa mpya zimeibuka kutokana na kilimohicho na kwamba wapo waliopata manufaa kutokakatika kilimo hicho cha alizeti kuanzisha shughurinyingine za 

kiuchumi ambazo pia zinamanufaamakubwa kwa maisha yao.

“ili kuondoa changamoto zilizopo kuna mambo kadhaayanatakiwa kufanyika, kwanza kuongeza huduma za ugani,upatikanaji wa pembejeo za kisasa,kuongeza 
tijakwa maeneo,kuwahakikishia wakulima masokokwakuwa soko na bei ndo kitu kinachowavutiawakulima kuzalisha zaidi kwakuwa wakiwa na uhakika wa 
kuuza kwa bei bora wanaweza wakavutiwa zaidikutumia mbegu za kisasa ambazo ni ghali kulinganishana mbegu za kienyeji lakini ambazo uzalishaji wake kwa 
tija ni mkubwa na ni mzuri “ alifafanua Profesa Jeckonia.

Mtafiti na Mkuu wa Mradi wa APRA, Profesa Aida Isinika kutoka SUA ameiomba NEMC kufuatilia ili kuhakikisha mazingira yanakuwasalama katika Wilaya ya Kilombero kutokana na matumizi mabaya ya viuatilifu hasa viua maguguyanayofanywa na wakulima  ambayo yasipodhibitiwayanaweza kuleta athari kwa afya zao na mazingira pia.

“Matumizi ya viau magugu yanawasaidia kupunguzakazi lakini matumizi yale yanatumika kwa njia ambayosi sahihi kwa hiyo inawezekana huko mbele 
tukapata matatizo makubwa” alieleza Profesa Isinika.

Aliongeza”si hivyo tu, kupanuka kwa Mashaba yampunga kuna athari kwenye mabwawa yanayotumikakutengeneza umeme hivyo tunaweza tukapanua lakini tukawa na madhara ya kufanya uharibifu kule hivyohayo ni mambo yanayotakiwa kufanyiwa kazi”. 

Utafiti umefanyika tangu mwaka 2017 naunategemewa kukamilika mapema mwakani na teyariumeshafanyika katika nchi sita ambazo ni Tanzania, Ethopia, Malawi, Zimbabwe, Ghana na Nigeria kwa kujikita kuchambua mmbo ya kisera yanayowezesha au kuhamasisha kilimo endelevu na shirikishi.

Hizo zote ni kujuhudi za kuboresha Maisha ya wadaukatika minyororo ya thamani ya kilimo ambapo kwahapa Tanzania utafiti huu uliratibiwa na watafiti kutokaChuo Kikuu Cha Sokoine cha Kilimo SUA  katikawilaya ya Kilombero wakijikita katika zao la mpungana wilaya za ikalama na Iramba kwa zao la alizeti.
 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments