MAHAKAMA YATUPILIA MBALI PINGAMIZI LA FREEMAN MBOWE NA WENZAKE


Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, leo Jumatano Oktoba 20, 2021 imetoa hukumu ya kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu ambapo imetupilia mbali mapingamizi mawili yaliyowasilishwa na upande wa utetezi.

Akisoma uamuzi huo, Jaji Mustapha Siyani ambaye kwa sasa ni Jaji Kiongozi, amesema mapingamizi yote mawili yamekosa mashiko, ambapo katika pingamizi la kwanza, mahakama imejiridhisha kwamba maelezo yalichukuliwa ndani ya saa nne zinazoruhusiwa kisheria na katika pingamizi la pili, mshtakiwa wa pili, Adam Kasekwa ‘Adamoo’ alitoa maelezo ya onyo kwa ridhaa yake.

Kwa uamuzi huo, maelezo ya mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo, Adamoo yamepokelewa kama kielelezo cha ushahidi wa upande wa mashtaka na sasa kesi ya msingi itaendelea kama kawaida.

Akisoma uamuzi huo Jaji Mustapha Siyani ameeleza kuwa anakubaliana na Jamhuri kuwa mazingira yaliyokuwepo yana mantiki kuwa walikuwa wakiendelea na upelelezi.

Amesema kuchelewa kuhojiwa kwake kulikuwa na sababu za kisheria chini ya kifungu cha 51(1) Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments