AJALI YA BASI LA ZACHARIA AIR NA PRADO YAUA WATU WAWILI TARIME


Watu wawili wamefariki dunia papo hapo, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana na Zakaria Air Bus uso kwa uso na Prado lenye namba T 184 AQT katika kijiji cha Gamasara, nje kidogo ya mji wa Tarime mkoani Mara.

Ajali hiyo imetokea leo Oktoba 3, 2021 - saa 3:15 asubuhi, wakati basi hilo lenye namba za usajili T 906 DLJ likitokea Mwanza na Prado lenye namba T 184 AQT likitokea mjini Tarime.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, waliofariki dunia na miili yao kupelekwa kuhifadhiwa chumba cha maiti katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tarime, ni ndugu kutoka familia moja ya kijijini Gamasara.

Taarifa zaidi zimeeleza kuwa baadhi ya abiria waliokuwa kwenye basi za Zakaria wamepata majeraha na kuwahishwa hospitalini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya, ACP William Mkonda amethibitisha kutokea kwa ajili hiyo, vifo vya watu wawili na majeruhi watatu.

"Vifo ni watu wawili na waliojeruhiwa ni watatu ambao tayari wamepelekwa hospitalini kupata matibabu," amesema Kamanda Mkonda 

CHANZO- MARA ONLINE BLOG

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments