Kimenuka! RC MJEMA AAGIZA DIWANI NA AFISA MTENDAJI WA TINDE WASHUGHULIKIWE KUPOTOSHA CHANJO YA UVIKO 19

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati wa kikao cha kamati ya afya ya msingi kuhusu tathmini ya utoaji wa chanjo dhidi ya Uviko 19 leo Oktoba 28,2021. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati wa kikao cha kamati ya afya ya msingi kuhusu tathmini ya utoaji wa chanjo dhidi ya Uviko 19 leo Oktoba 28,2021.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema ameagiza mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua za kinidhamu Diwani wa Kata ya Tinde halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Jafari Kanolo na Afisa Mtendaji wa Kata ya Tinde Latifa Mwendapole kwa kufanya upotoshaji kuhusu Chanjo ya Uviko - 19.

Mhe. Mjema ametoa agiza hilo leo Oktoba 28,2021 wakati wa kikao cha kamati ya afya ya msingi kuhusu tathmini ya utoaji wa chanjo dhidi ya Uviko 19 kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa pia na wadau mbalimbali wa afya.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema wapo baadhi ya wanasiasa na viongozi ambao wapo mbele kusema chanjo ya COVID haitafanikiwa na kuhamasisha watu wasipate chanjo kitendo ambacho ameeleza kuwa hatakubali kuona kinaendelea mkoani Shinyanga.

"Diwani wa kata ya Tinde na Afisa Mtendaji wa kata ya Tinde wanatukwamisha kwa kufanya upotoshaji kuhusu Chanjo dhidi ya Covid 19 .Naagiza hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yao
 na hii iwe fundisho kwa watu wengine, hatuwezi kuona watu wanapotosha tukawaacha hivi hivi”,amesema Mjema.

“Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameleta chanjo ya UVIKO 19 ili wananchi wapate kujinusuru dhidi ya ugonjwa wa Corona. Mhe. Rais kaleta chanjo ili wananchi wawe salama. Rais anapotoa chanjo hizi, anapoleta chanjo anataka maendeleo”,amesema Mjema.

“Tumemaliza chanjo ya COVID 19 awamu ya kwanza lakini awamu ya pili chanjo zingine zimeletwa, wale ambao hawajapata chanjo naomba wajitokeze wapate ili kujinusuru na Uviko 19”,ameongeza.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati wa kikao cha kamati ya afya ya msingi kuhusu tathmini ya utoaji wa chanjo dhidi ya Uviko 19 leo Oktoba 28,2021. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akiongoza kikao cha kamati ya afya ya msingi kuhusu tathmini ya utoaji wa chanjo dhidi ya Uviko 19 leo Oktoba 28,2021.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Zuwena Omary akizungumza katika kikao cha kamati ya afya ya msingi kuhusu tathmini ya utoaji wa chanjo dhidi ya Uviko 19 leo Oktoba 28,2021.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Danny Mzee akizungumza katika kikao cha kamati ya afya ya msingi kuhusu tathmini ya utoaji wa chanjo dhidi ya Uviko 19 leo Oktoba 28,2021.
Mratibu wa Chanjo ya Uviko 19 Mkoa wa Shinyanga, Timoth Sosoma akizungumza katika kikao cha kamati ya afya ya msingi kuhusu tathmini ya utoaji wa chanjo dhidi ya Uviko 19 leo Oktoba 28,2021.


Wadau wakiwa katika kikao cha kamati ya afya ya msingi kuhusu tathmini ya utoaji wa chanjo dhidi ya Uviko 19 leo Oktoba 28,2021.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments