Breaking

Post Top Ad

Tuesday, October 26, 2021

AMUUA MMILIKI WA PAKA BAADA YA PAKA KUZINGUA
Unaambiwa huko Florida, jamaa mmoja anayejulikana kwa jina la Cliffton Bliss Jr (58) anashtakiwa kwa kosa la kumuua kwa risasi jirani yake James Taylor Jr (41) , ambaye alikuwa ni mmiliki wa paka.

Cliffton alifanya mauaji hayo baada ya kukasirishwa na paka wa jirani huyo aliyeingia ndani ya chumba chake, taarifa za polisi zinasema Cliffton alishika bunduki yake na kutishia kumuua paka huyo lakini mmiliki wa paka akamsihi asifanye hivyo, na hapo ndipo Cliffton alipogeuza uelekeo wa bunduki yake na kumpiga mmiliki wa paka na kupelekea kifo chake.

Uchunguzi bado unaendelea, lakini mshtakiwa alijitetea kwamba alitekeleza mauaji hayo baada ya kushambuliwa kwa matusi na mmiliki wa paka huyo!

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages