MPIGA PICHA AFUTA PICHA ZA BWANA HARUSI BAADA YA KUNYIMWA CHAKULA NA VINYWAJI


Mpiga picha mmoja ametofautiana vikali na mwajiri wake na kuamua kufuta picha zake zote ambazo alikuwa amempiga pamoja na mke wake.

Mpiga picha huyo alikuwa amekodishwa na rafiki yake ambaye alikuwa na sherehe ya harusi ampige picha  na amedai kuwa  hakuruhusiwa kupumzika wakati wa hafla hiyo kwani alikuwa anatakiwa kupiga picha kuanzia kati ya saa tano asubuhi hadi saa moja usiku.

Akitoa malalamishi yake kupitia mtandao wa Reddit, tovuti maarufu ya Marekani, mpiga picha huyo alikuwa amekodishwa na rafiki yake ambaye alikuwa na sherehe ya harusi ampige picha. 

Alisema huduma zake hazijawahi kukodishwa mbeleni na bwana harusi huyo alimtafuta sababu ya gharama yake ya chini.

Mpiga picha huyo baada ya kushawishiwa, aliamua kuchukua kibarua hicho na kuwasili mapema katika harusi ya swahiba wake kuchapa kazi.

Akiwa amejihami na vifaa vyake, alianza kazi saa tano asubuhi na alikuwa ameratibiwa kumaliza kufikia saa moja usiku.

Katika hafla hiyo, wakati wa chakula uliwadia na kila mgeni alikuwa akipakuliwa.

 Mpiga picha huyo alijaribu kujumuika na wengine kwa chakula lakini alizuiwa na bwana harusi akihoji kuwa anatakiwa kupiga picha ya hafla nzima bila kusita wala kupumzika. 

Alisema alikuwa amechoka tiki, na kile alihitaji ni kupumzika na angalau kupata kopo la maji ambalo alinyimwa.

Bwana harusi alimtishia kuwa hatamlipa iwapo atapumzika.

 “Nilimwambia bwana harusi kuwa nahitaji kupumzika kwa dakika 20 angalau kupata chakula na maji.Lakini bwana harusi aliniambia kuwa natakiwa kuwa mpiga picha ama niondoke bila kulipwa," aliandika mpiga picha huyo. 

Mpiga picha hiyo alikasirika na kumuomba bwana harusi iwapo anaweza kufuta picha zote ambazo alikuwa amezipiga siku hiyo.

 Bwana harusi alikubali na kisha mpiga picha huyo alifuta picha zote kabla ya kuondoka akiapa kutowahi kujihusha tena na hafla za bwana harusi huyo.

 Alisema pesa ambazo alikuwa anatazamia kulipwa zilikuwa kidogo na za kudunisha thamani yake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments