WANAJESHI WANNE WA JESHI LA RWANDA WAUAWA MSUMBIJI | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, September 29, 2021

WANAJESHI WANNE WA JESHI LA RWANDA WAUAWA MSUMBIJI

  Malunde       Wednesday, September 29, 2021


Maofisa wanne wa jeshi la Rwanda wameuawa nchini Msumbiji, katika operesheni ya kijeshi dhidi ya wanamgambo wa kiislamu, katika jimbo la Cabo Delgado.

Taarifa kutoka nchini Rwanda zinasema, wanajeshi wengine 14, wamejeruhiwa vibaya katika mapigano hayo.
 

Hii ni mara ya kwanza kwa Rwanda kutangaza majeruhi katika kikosi chake cha wanajeshi 1,000 kilichopo nchini Msumbiji, tangu waanze operesheni ya kukabiliana na wanamgambo hao.

Haijawekwa wazi ni katika eneo gani haswa la jimbo la Cabo Delgado, ambako wanajeshi wa Rwanda waliuawa.

Jumamosi iliyopita, marais wa Msumbiji – Filipe Nyusi na wa Rwanda, Paul Kageme – waliwapongeza wanajeshi ambao wamejitoa kupambaa na magaidi.

Rwanda imepeleka nchini humo wanajeshi 1,000 kukabiliana na wapiganaji hao wanafanya mashambulizi ya uharibifu kaskazini mwa taifa hilo.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post