WAKURUGENZI WATAKIWA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS SAMIA KUHUSU WAMACHINGA
Saturday, September 25, 2021
Wakurugenzi wa halmashauri nchini wametakiwa kutekeleza agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la kuwapanga wamachinga kutekelezwa bila kutumia mabavu.
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ummy Mwalimu wakati wa akifungua kikao kazi cha siku mbili na wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Alisema ni vyema wakatumia mwezi mmoja uliotolewa kuwaelimisha na kuwashirikisha wamachinga katika kupanga miji.
Septemba 13 mwaka huu, Rais Samia Suluhu Hassan alitoa maelekezo Kwa halmashauri za Majiji na manispaa kuwapanga wamachinga na Waziri Mkuu alitoa maelekezo ya kutekeleza hilo ndani ya mwezi mmoja.
Alisema Wakurugenzi wanapaswa kuwa makini na njia wanazozitumia kuwatoa wamachinga kuwa ziwe ni zile zinazingatia utu, heshima na thamani ya wafanyabiashara wadogo wadogo.
“ Nataka kusisitiza tutumie mwezi mmoja huu kutoa elimu Kwa wamachinga na kuhakikisha wanashirikishwa katika kupanga miji.”
“ Tujitahidi sana kutotumia nguvu na mabavu, tutekeleze maagizo ya Rais huku tukizingatia sheria, taratibu na kanuni na kuwashirikisha na kuandaa maeneo ya kuwapeleka.”
Ummy pia aliwataka kutengwa maeneo ya wafanya biashara ambayo wananchi wanafika kiurahisi
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com
🚧🚦 Usiendeshe gari lako bila Mafunzo na Leseni halali_ 📲 Wasiliana nasi sasa: wa.me/255740273285 Unahitaji nini? 🚘 Unataka kujifunza udereva wa magari na kupata Cheti? 📄 Una cheti unataka kupata Leseni? 🔄 Unajua kuendesha lakini huna cheti wala leseni na unataka refresh upate cheti? 🛣️ Una nyaraka zote muhimu lakini unahitaji kujifua zaidi barabarani? ✅ Una Leseni bila cheti na unataka renew? 🌍 Tupo mikoa yote Tanzania hadi vijijini! 📞 Tupigie sasa: 0769 763 285
Social Plugin