KIJANA AUAWA KWA VISU KISHA KUNING'INIZWA JUU YA MTI WA MPARACHICHI - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Thursday, September 30, 2021

KIJANA AUAWA KWA VISU KISHA KUNING'INIZWA JUU YA MTI WA MPARACHICHIKijana Melkezedik Robert mwenye umri wa miaka 35, mkazi wa kijiji cha Nyerezi, Arumeru mkoani Arusha, amekutwa amekufa huku mwili wake ukiwa umening’inizwa juu ya mti ya mparachichi.

Mwenyekiti wa ulinzi wa wa Kitongoji cha Achi, aliyejitambulisha kwa jina moja la Agesmun, amesema walikuta mwili wa kijana huyo ukiwa umekatwakatwa visu katika maeneo mbalimbali mgongoni.

Alisema mara baada ya polisi kufika, waliwashikilia baba na mdogo wa marehemu ambaye inasadikika alikuwa na ugomvi na marehemu kaka yake.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages