POLISI WASEMA UCHUNGUZI UNAONESHA JAMAA 'Hamza' ALIYEUA ASKARI KISHA KUUAWA DAR ALIKUWA GAIDI | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, September 2, 2021

POLISI WASEMA UCHUNGUZI UNAONESHA JAMAA 'Hamza' ALIYEUA ASKARI KISHA KUUAWA DAR ALIKUWA GAIDI

  Malunde       Thursday, September 2, 2021

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura amesema, uchunguzi uliofanywa na Jeshi la Polisi kuhusu Hamza Mohamed aliyewaua askari  watatu wa Jeshi la Polisi na mlinzi mmoja wa kampuni ya SGA kisha naye kuuawa Jijini Dar es salaam umebaini kwamba Hamza Mohamed alikuwa ni gaidi wa kujitoa mhanga.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza leo Septemba 2, 2021, Wambura amesema uchunguzi uliofanywa na polisi umebaini kwamba Hamza alikuwa akiishi kisiri huku akiwa amegubikwa na viashiria vyote vya ugaidi na kwamba alikuwa akijifunza mambo ya kigaidi kupitia mitandao ya kijamii ambayo kwa kipindi kirefu amekuwa akifuatilia mitandao inayoonyesha matendo ya Al-Shabab na makundi kama ISIS.

Ameongeza kuwa taarifa zinazodai kwamba Hamza aliwashambulia askari hao kwa sababu walimdhulumu madini yake, si za kweli kwa sababu uchunguzi umebaini kwamba hakuwa na madini wala fedha na kwamba umiliki wake wa mgodi wa dhahabu Chunya, ulisimama kwa muda mrefu.

CHANZO - Mpekuzi Blog

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post