JAKAYA KIKWETE : MPAKA SASA RAIS SAMIA ANAENDESHA NCHI VIZURI



Rais mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete amempongeza Rais Samia Suluhu na kusema anaendesha nchi vizuri na kwamba changamoto hazikosekani.

Kikwete ameyasema haya leo Jumanne, Septemba 14, 2021 mbele ya Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel walipotembelea eneo kutakakojengwa mradi wa jengo la matibabu ya dharura kwenye Hospitali ya Wilaya ya Chalinze iliyopo Msoga ukiwa ni mradi unaofadhiliwa na ABBOTT FUND ya Marekani kwa gharama ya Bilioni 1.2.

“Tuendelee kumuunga mkono Rais wetu, anayo dhamana kubwa, sio kazi rahisi, ina mawimbi mengi na pengine kwenye kazi ile unapata siku za furaha ni kidogo kuliko siku za maudhi lakini cha umuhimu ni wewe kuwa na moyo wa uvumilivu na ustahimilivu.

“Mpaka sasa anaendesha nchi vizuri changamoto hazikosekani, nilisema wakati mmoja kwamba Babu yangu alinisumulia kwamba nchi haipoi kama ugali, ugali ukichelewa kuula unapoa wote, nchi siku zote haiwi hivyo, hapa pakipoa mara kunaibuka hili mara lile lakini katika yote hayo mpaka sasa analiongoza Taifa vizuri.


“Uongozi atapata moyo zaidi akiona sisi ambao tupo pamoja nae tunaendelea kumuunga mkono kumuonesha kwamba tupo pamoja, ukiwa pamoja na wenzako unapata moyo wa kukabiliana na changamoto kubwa zilizopo ofisini,” amesema Kikwete.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments