CRDB KUJENGA GETI LA KISASA CHUO KIKUU CHA DODOMA - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Tuesday, September 28, 2021

CRDB KUJENGA GETI LA KISASA CHUO KIKUU CHA DODOMA

 
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof. Faustine Bee (kushoto) na Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts wakibadilishana nyaraka za mkataba wa makubaliano ya ujenzi wa geti kuu la kisasa katika chuo kikuu cha UDOM. CRDB itajenga geti hilo kwa gharama ya shilingi milioni 150.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof. Faustine Bee (kushoto) na Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts wakisaini mkataba wa makubaliano ya ujenzi wa geti kuu la kisasa katika chuo kikuu cha UDOM. CRDB itajenga geti hilo kwa gharama ya shilingi milioni 150. 
Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts akiweka muhiri katika mkataba huo na Chuo Kikuu cha UDOM. 
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof. Faustine Bee, akisaini mktaba huo na CRDB leo Septemba 28,2021 ambapo benki ya CRDB itajenga geti la kisasa la chuo hicho katika barabara ya kuingia Chuoni hapo kwa gharama ya shilingi Milioni 150. 
Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts akizungumza kuhusu mkataba huo ambapo alisema Benki ya CRDBAlisema CRDB imebaini maeneo matatu makubwa ambayo imeamua kuwekeza ili kurejesha mapato yake kwa jamii  ambayo ni elimu afya na mazingira.

Makamu Mkuu wa Chuo cha UDOM Profesa Faustine Bee akizungumza na kusema kukamilika kwa geti hilo litaboresha muonekano wa chuo na kuimarisha usalama wa wanafunzi na mali zao.

Baadhi ya watumishi wa CRDB walioshiriki na kushuhudia utiaji saini wa makubaliano hayo. 
Picha ya Pamoja kati ya viongozi wa CRDB na Chuo Kikuu cha Dodoma.
************
Benki ya CRDB kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma zimeingia makubaliano kuanza kwa ujenzi wa geti la kisasa kuingilia ndani ya chuo litakaloghalimu shilingi  Milioni 150 lengo kuimarisha usalama.

Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo, Afisa Biashara Mkuu wa Benki ya CRDB,  Dk Joseph Witts amesema geti litakalojengwa litakuwa kubwa kuliko mageti yote ambayo yaliwahi kujengwa katika vyuo vikuu vyote hapa nchini.

Alisema CRDB imebaini maeneo matatu makubwa ambayo imeamua kuwekeza ili kurejesha mapato yake kwa jamii  ambayo ni elimu afya na mazingira.

"Katika sekta ya elimu tumeamua   kuwapatia wanajamii fadhila kwa  Kuchangia ujenzi wa geti ambalo halijawahi kutokea hapa nchini  na CRDB tumezamini  na itagharimu zaidi ya sh.milion 150 na zimetolewa kama sehemu ya kurudisha mchango wake," alisema Dk Witts.

Alisema geti hilo litasaidia kuwawekea wanafunzi mazingira mazuri ya kusoma na baadae waje kuwa viongozi wakubwa hapa  nchini.

Nae Makamu Mkuu wa Chuo cha UDOM Profesa Faustine Bee alisema kukamilika kwa geti hilo litaboresha muonekano wa chuo na kuimarisha usalama wa wanafunzi na mali zao.

“Tunawashukuru wenzetu wa benki ya CRDB kwa kuona umuhimu wa kutuchangia maboresho haya ambayo tulitamani yatokee na katika kurudisha shukrani kwa jamii katika sekta ya elimu wakaamua kujenga geti la chuo chetu nawapongeza sana,”alisema Prof Bee.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages