BONDE LA WAMI/RUVU:MAJI YA MTO RUVU YAMEPUNGUA , VIBALI VYA UVUNAJI MAJI VYASITISHWA. | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, September 15, 2021

BONDE LA WAMI/RUVU:MAJI YA MTO RUVU YAMEPUNGUA , VIBALI VYA UVUNAJI MAJI VYASITISHWA.

  sayarinews.co.tz       Wednesday, September 15, 2021

Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Bonde la Wami Ruvu Elibariki Mmasi akizungumza na waandishi wa habari katika Daraja la Ruvu baada kwenda kuangalia kupungua kwa maji na kutoa tahadhari juu shughuli kibinadamu katika Mto huo.

Sehemu ambayo Dawasa inachukua maji ambapo ni Lita 5000 kwa sekunde kutokana na maji hayo kupungua

Sehemu maji katika Mto Ruvu yanavyoonyesha kupungua kwa mwaka huu.

***********************************

Na Mwandishi Wetu

Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu imesema kuwa kwa kipindi hiki imesitisha vibali vyote vya uvunaji maji katika Mto Ruvu pamoja na kuwataka wananchi kuacha shughuli za kibidamu katika mto huo.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Bonde la Wami/Ruvu Elibariki Mmasi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Daraja la Mto Ruvu mkoani Pwani,Mmasi amesema kuwa kina cha maji kimepungua ikilinganishwa na Septemba 14 ya mwaka jana iliyokuwa na Kina cha mita 12500 hadi kufikia mita 7500 ambapo Mamlaka ya Mazingira na Maji Safi na Maji taka (DAWASA) katika kidakio cha Ruvu Juu inachukua milimita 5000 kwa sekunde.

Mmasi amesema kupungua kwa kina hicho kwa kuendelea shughuli zingine za binadamu kinaweza kiendelea kupungua na kuleta adha kwa watumiaji maji majumbani.

Mmasi amesema Bodi ya Bonde la Wami/Ruv haiwezi kuruhusu kuendelea shughuli za kibinadamu wakati mazingira ya kulinda vyanzo vya maji vimewekwa kwa kuweka shughuli za kibindamu ikiwemo ufugaji nyuki pamoja kuwachimbia visima.

Aidha amesema wanachoombea mvua zianze kunyesha mapema kuchelewa kwa mvua hizo kunaweza kufanya wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam kupata maji kidogo.

Amesema kuwa kutokana na hali hiyo wameendelea kudhibiti maji vyanzo kwa maeneo baadhi ya mito maji ya yamechepuka hovyo wanarudisha pamoja na ujenzi wa bwawa Dunda ambapo maji yakipungua Bwawa ndilo litakuwa linatumiika.

Hata hivyo amesema utunzaji wa vyanzo vya maji la wote kwani kuacha vynzo hivyo vitatumika kiholela madhara yake ni makubwa sana.

Mmasi amesema kuwa kuna faini zipo kutokana na sheria zilizowekwa katika utunzaji wa vyanzo maji kuanzia laki tatu hadi sh.milioni 50 na baada ya hapo kufungulia mashitaka.

Aidha Mmasi amesema kazi vyanzo vya maji viangaliwe kwa macho mawili kukosekana kwa maji madhara yake ni makubwa hivyo kila jamii iliyopo katika vyanzo hivyo kuwa na wajibu huo.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post