MO DEWJI AJIUZULU UENYEKITI SIMBA SC....TRY AGAIN ABEBA MIKOBA - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Wednesday, September 29, 2021

MO DEWJI AJIUZULU UENYEKITI SIMBA SC....TRY AGAIN ABEBA MIKOBA


Mohammed Dewji ''MO''

Mwekezaji wa klabu ya Simba SC Mohammed Dewji amejiuzulu nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo na nafasi yake imechukuliwa na Abdallah Salim maarufu Try Again.

Mo ameitumikia nafasi hiyo kwa miaka 4 na ameweka wazi kuwa uamuzi huo ulifikiwa kwenye kikao cha bodi kilichofanyika Septemba 21 2021.

Katika taarifa yake aliyoiweka katika mashindano ya kijamii ,Dewji amesema sababu za yeye kujiuzulu ni kutokana na kutokuwepo nchini muda mwingi na anaamini anahitajika Mwenyekiti ambaye atakuwepo nchini muda wote.

Lakini pia ameweka wazi kujiuzulu kwake kwenye nafasi hiyo hakumaanikishi kuwa katoka kabisa, lakini anabaki kama mwekezaji na mwanahisa, na kwa sasa atajikita zaidi kwenye soka la vijana na kuboresha miundo mbinu ya klabu hiyo.

Tajiri huyo akiwa Mwenyekiti wa bodi ya Simba, Klabu hiyo imeshinda mataji 4 ya Ligi Kuu, makombe 2 ya kombe la Azam Sports Federation CUP lakini pia Simba ilifanikiwa kufika hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa barani Afrika mara mbili ndani ya misimu mitatu iliyopita.

Via EATV

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages