MWANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE AUAWA BAADA YA KUFUMANIWA AKIHONDOMOLA MKE WA MTU


Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Kapsumbeiywo huko Kuresoi Kusini, Kaunti ya Nakuru nchini Kenya ameuawa baada ya kupatikana na mwanamke wa wenyewe.

Mvulana huyo wa miaka 19 amepoteza maisha yake baada ya kupatikana akionja asali ya mwanamke wa miaka 35.

Wawili hao walipatikana nyumbani kwa mwanamke huyo na mumewe aliyeshikwa na hasira na kumkatakata vipande vipande kwa panga kijana huyo.

Akithibitisha kisa hicho, DCIO wa Kuresoi Peter Obonyo alisema mwanafunzi huyo alifariki dunia akipokea matibabu katika hospitali ya Nakuru Level Five.

 Kachero wa uchunguzi Kuresoi Peter Obonyo alisema Japheth Bii alimpata kijana huyo kwenye kitanda chake na mkewe wakifanya mapenzi.

Alisema mwanafunzi huyo alikimbizwa katika hospitali ya kaunti mjini Nakuru baada ya kisa hicho lakini akafariki dunia.

 “Edmond Kipng’etich wa miaka 19 ambaye ni mwanafunzi alipatikana nyumbani kwa Bii ambapo alikuwa akionja tunda la mkewe Judy Chelang’at wa miaka 35. Bii alimshambulia ndani ya nyumba lakini kijana huyo akaokolewa na wananchi,” taarifa ilisema.

Baada ya kuokolewa, kijana huyo alikimbizwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Olenguruone lakini hali ikawa mbaya na kukimbizwa Nakuru.

Obonyo amewaonya wanaume dhidi ya kuingia kwenye mtego wa wake wa wenyewe akisema ni hatari sana. Polisi wanamsaka Bii ambaye aliingia mafichoni baada ya kumshambulia mwanafunzi huyo.

 Kisa hicho kimewaacha wakazi kinywa wazi huku wakishangaa ni vipi kijana huyo alifaulu kumteka mwanamke aliyekomaa kimapenzi.


Polisi wameanzisha msako dhidi ya mshukiwa huyo kwa jina kwa jina Japheth Bii ambaye anasemekana aliingia mafichoni baada ya kisa hicho cha kusikitisha.

Kwingineko jamaa mmoja alipoteza maisha yake baada ya kushambuliwa kwa kisu na mwenzake aliyempata katika boma lake eneo la Kagoto, kaunti ya Nakuru.

Maafisa wa polisi katika uchunguzi wao walisema kwamba kisa hicho kilitokea baada ya mshukiwa kupandishwa hasira na marehemu.

Vurugu hizo zilianza wakati Micah Nyaberi Bogomba aliporudi kwake ghafla saa tisa usiku Jumamosi, Agosti 28 na kumkuta jamaa huyo mwenye umri wa miaka 34 akijistarehesha kwake.

Nyaberi, mwenye umri wa miaka 39, alikuwa na hasira na alitaka kujua ni biashara gani haswa ilikuwa inaendelea kati ya Boniface Njagi Maina na mkewe Harriet Vivian Mboga.

Kabla ya mwenda zake kutamka lolote, mshukiwa alimrukia kwa ngumi nzito na mateke.

Kulingana na mashuhuda, Njagi ambaye alikuwa akihofia maisha yake aliripotiwa kumsihi Nyaberi amruhusu achukue viatu vyake na kuondoka, lakini ombi lake liliambulia patupu kwani alidungwa kisu begani.

Polisi kutoka Kituo cha Doria cha Kagoto walifika mara moja eneo la tukio na kuupata mwili wa Njagi ukiwa umelala kwenye damu iliyotapakaa katika lango la boma hilo. Katika nyumba ya mtuhumiwa, polisi pia walipata damu kwenye kuta na vifaa vya nyumbani, ambavyo vitatumika kwa ushahidi.

Washukiwa wawili Micah Nyaberi Bogomba na Harriet Vivian Mboga Musumba walikamatwa na kukabidhiwa kwa maafisa wa upelelezi wa DCI Nakuru Kaskazini ili wachukuliwe hatua za kisheria. Mwili wa mwenda zake ulipelekwa katika makafani moja ya eneo hilo.

CHANZO - TUKO NEWS

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post