TAARIFA KWA UMMA: MAKATO KODI YA MAJENGO KWA KUTUMIA NJIA YA UMEME (LUKU) KUANZA KESHO

 Utekelezaji wa ukusanyaji wa kodi ya majengo kwa kutumia njia ya umeme (LUKU), utaanza rasmi kesho Agosti 20, 2021, na kwamba utahusisha mita za umeme za aina zote ambapo kila mnunuaji wa umeme atakatwa 1,000 kwa mwezi kwa nyumba ya kawaida na 5,000 kwa mwezi kwa kila sakafu ya ghorofa.

Utekelezaji wa sheria hiyo mpya ya kodi utafanyika kwa usimamizi wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), na TANESCO ambapo viwango hivyo kwa sasa ni shilingi 12,000 kwa jengo la kawaida kutoka 10,000 iliyokuwa ikitozwa hapo awali na shilingi 60,000 kwa kila sakafu moja ya ghorofa kutoka 50,000 ya awali.

Taarifa ya Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kitada imesema utaratibu wa makato ya kodi ya jengo kwa mfumo huo, imekuja kufuatia marekebisho ya sheria ya kodi ya mamlaka ya serikali za mitaa iliyopitishwa na BUnge la Bajeti mwaka 2021, ambapo viwango vya kodi vimebadilishwa.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments