SERIKALI IMEKUSUDIA KUWEKA VITENDEA KAZI VYA KUPIMA MAGARI MAKUBWA (SCANNER) NA KUDHIBITI MIZIGO INAYOPITA KATIKA MIPAKA YA NCHI YETU.



Naibu waziri wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) akipata maelezo alipotembelea kituo cha pamoja cha ushuru wa forodha mipakani (OSBP) kilichopo Namanga Mkoani Arusha.

Kamati ya kudumu ya Bunge ya bajeti Mhe. Daniel Sillo Baran Mbunge wa Babati Vijijini akipata maelezo katika ziara aliyoambatana na kamati ya kudumu ya bunge kutembelea kituo cha pamoja cha ushuru wa forodha mipakani (OSBP) kilichopo Namanga Mkoani Arusha.


Kamati ya kudumu ya bunge ikiwa katika ziara ya kutembelea utendaji wa kituo cha pamoja cha ushuru wa forodha mipakani (OSBP) kilichopo Namanga.


Picha ya pamoja ya kamati ya kudumu ya bunge waliyopiga wakiwa katika eneo la nchi ya Kenya walipotembelea kituo cha pamoja cha ushuru wa forodha mipakani (OSBP) kilichopo Namanga Mkoani Arusha.


Gari maalumu lililopo upande wa nchi ya Kenya linalotumika kupima magari makubwa (Scanner) kudhibiti mizigo inayovuka mpakani Namanga.


Muonekano wa kituo cha pamoja cha ushuru wa forodha mipakani (OSBP) kwa upande wa nchi ya Kenya kilichopo Namanga.


Naibu Waziri Mhe. Exaud Kigahe (Kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa Kiwanda cha kuchakata nyama cha Eliya Foods Overseas Ltd ndugu Shabbir Virjee, katikati ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Bishara Dkt. Hashil T. Abdallah.

***************************

Naibu waziri Mhe. Kigahe ameyasema hayo leo alipotembelea kituo cha pamoja cha ushuru wa forodha mipakani (OSBP) kilichopo Namanga Mkoani Arusha akiwa ameambatana na Kamati ya kudumu ya Bunge ya bajeti.

Mhe. Kigahe amesema kuwa nia ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha inatatua changamoto zilizopo katika mipaka yetu ili kuchochea upatikanaji wa mapato na kurahisisha biashara.

“Serikali imekusudia kuweka vitendea kazi vya kupima magari makubwa (Scanner) na kudhibiti mizigo pamoja na kuondosha changamoto za msongamano wa magari na upimaji wa ugonjwa wa UVIKO 19” Amesema Mhe. Kigahe.

Mhe. Kigahe ameishukuru kamati ya kudumu ya bunge ya bajeti kwa ushirikiano walioutoa kwa wizara ya viwanda na biashara hasa kutembelea miradi mbalimbali ya kimkakati na kutoa maoni yao ya kuboresha maeneo husika.

Naye Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya bajeti Mhe. Daniel Baran Sillo (Mb) amesema kuwa uongozi wa wizara ya Viwanda na Biashara umetoa ushirikiano mkubwa kwa kamati anayoiongoza na waheshimiwa wabunge wamejionea na kusikiliza changamoto zote hivyo kamati yake itakaa na kufanya uchambuzi na kuishauri serikali namna bora ya kuboresha na kutatua changamoto zilizopo.

Kamati ya kudumu ya bunge imepata fursa nyingine ya kutembelea kiwanda cha kuchakata nyama cha Eliya Foods Overseas Ltd kilichopo Longido Mkoa wa Arusha, kiwanda hiki kipo chini ya EPZA kikichakata nyama kwa ajili ya mauzo nje.

Mwenyekiti wa kiwanda hiki ndugu Shabbir Virjee amelishukuru bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye kupunguza kodi ya nyama ambayo imesaidia katika ushindani na nchi nyingine.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post