KAULI YA NDUGAI KUHUSU WABUNGE WANAOPINGA CHANJO YA CORONA HADHARANI


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai

Spika wa Bunge Job Ndugai, ametoa kauli kuwa subira yavuta kheri hivyo tuendelee kungoja huenda zipo hatua zitakazochukuliwa na Bunge hilo kwa wabunge ambao wametoa kauli zao hadharani kwamba hawapo tayari kuchoma chanjo Corona.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Agosti 12, 2021, alipowasiliana na East Africa Radio na EATV Digital, alipoulizwa swali kuhusu hatua zitakazochukuliwa kwa wabunge hao akiwemo Humphrey Polepole na Askofu Josephat Gwajima waliotoa kauli hizo, kwa kuwa vikao vya Bunge hilo vinatarajia kuanza mwishoni mwa mwezi huu.

"Subira yavuta kheri, tusubiri," amejibu Spika Ndugai.

Via EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments