HAJI MANARA AFUNGUKA MAMBO MAZITO BAADA YA KUONDOKA SIMBA

Aliyekuwa msemaji wa Simba Haji Manara amevunja ukimya na kueleza sababu zilizomtoa klabuni hapo na nafasi yake kupewa Ezekiel Kamwaga.

Manara ambaye alihudumu katika timu hiyo kwa zaidi ya miaka sita ameeleza sababu za kutolewa katika nafasi hiyo huku akitaja ni sababu za kibiashara na umaarufu.

Alisema kuwa licha ya kufanya kazi kwa miaka sita katika timu hiyo bila mkataba ila alijitolea vya kutosha kutokana na mapenzi yake kwenye klabu hiyo licha ya kudai kupewa tuhuma alizodai kuwa hazipo.

“Nimefanya kazi ya kujitolea kwenye hii klabu mpaka kufikia hatua ya kusafiri kwa gharama zangu mwenyewe bila hata kupewa na uongozi, hii ni kuonyesha kabisa ni jinsi gani uongozi wa sasa umekuwa ukinifanyia vitu vya kinyama na nisivyotarajia.

“Sina mkataba kwa miaka sita watu wanakuja wanapewa mikataba mie naachwa, sina promotion, laki saba hiyo hiyo imesimama kama mbuyu tangu 2015, nilikubali kwa sababu ni Simba yangu. Naipenda hii klabu namwachia nani?

“Wakati Senzo anakuja kwa mara ya kwanza, alinifuata na kuniambia amepewa kazi ya kunifukuza Mimi kazi, lakini Senzo alihoji kwanini nimfukuze bila sababu?

“Kifupi walimleta Senzo ili atekeleze matakwa ya wakubwa ila Senzo alisimama imara sana, alipinga kufanya kitu bila kukichunguza ndicho kilichomuondoa Simba.

“Simba inacheza nje ya Dar, msemaji wa timu sikatiwi tiketi. Naenda kwa kujitegemea nauli na hoteli. Hadi mechi za nje ya nchi. Nilishawahi kwenda South Africa kwa nauli yangu klabu ilishindwa kunilipia hata hotel, Nikalala kwenye kochi.

“Shida zote nilizopata na Simba, hawa watu hawaniheshimu, hawana mkataba na mimi. Majungu yote wananifanyia sasa leo wananipa jungu jipya la kuhujumu yani mimi nikahujumu Simba? Nahujumu vipi naenda kwenye camp ya Yanga? Nawaambiaje?

“Kuna siku Mohammed Dewji ‘MO’ alininipigia simu akaniambia watu wananilalamikia kuwa wewe umekuwa maarufu kunizidi mimi. Nikamwambia mie nitafanyeje? Nitawazuia watu? Kwani najipa mwenyewe umaarufu? Akaniambia watu wanasema tukutoe nikamwambia nitoeni

“Kwa nini leo sipo Simba? Sababu ni mbili, biashara na umaarufu. Haji ameathirika na hayo mambo mawili. Ndiyo maana unasikia inarudiwa mara nyingi kwamba hakuna mtu mkubwa zaidi ya klabu, lini mimi nimesema ni mkubwa kuliko klabu?” Amesema ManaraDownload/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments