BABA NA MTOTO WADAIWA KUMUUA MAMA BAADA YA KUCHOKA KUMUUGUZA TABORA | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, August 5, 2021

BABA NA MTOTO WADAIWA KUMUUA MAMA BAADA YA KUCHOKA KUMUUGUZA TABORA

  Malunde       Thursday, August 5, 2021
Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 57 mkazi wa kata ya Puge wilaya ya Nzega mkoani Tabora ameuawa na kisha kuning'inizwa kwenye kamba ili aonekane amejinyonga.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Tabora ACP Sophia Jongo amesema tukio hilo limetokea Agosti 4, 2021 katika kijiji cha Isalalo tarafa ya Puge ambapo baba na mtoto wake wanatuhumiwa kumuua na kutengeneza tukio la kujinyonga.

Amesema Jeshi la polisi mkoani Tabora linawashikilia watu watatu wakiwemo mume na watoto wake wawili kwa kula njama za kuumua mama yao na mume kuumua mkewe aliyetambulika kwa jina la Maria Kishiwa baada ya mwanamke huyo kuugua maradhi kwa muda mrefu waliona kero hivyo wakalazimika kummalizia mbali mama huyo.

Amesema chanzo ni kuugua maradhi kwa muda mrefu na mbinu iliyotumika ni kumfanga kamba shingoni na kumninginiza ili aonekane kuwa amejinyonga.

Amesema Maria alikuwa amefariki akiwa amefungwa kamba shingoni huku akining'inia na kamba ikiwa imefungwa kwa kukazwa kwenye nguzo ya jiko kitu ambacho marehemu hakuwa na nguvu kiasi hicho baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Hata hivyo kamanda huyo wa polisi amesema kwamba baada ya kumning'iniza marehemu waliacha kinu na kigoda bila kuanguka chini ili kuonyesha kuwa ndipo alipopanda na kujinyonga.

“Wakati ni vigumu kwa mtu mgonjwa kupanda hadi kuwe na msaada wa watu wengine jambo ambalo lilileta mashaka", amesema kamanda Safia.

Amesema marehemu Maria alikuwa analala na mjukuu wake ambaye alifichwa ili asibaini mbinu hiyo ya mauaji jambo hilo ndilo lilipelekea polisi kuanza kuchunguza ambapo mjukuu huyo alisema kila kitu kilichofanyika kumuua bibi yake.

Ameeleza kuwa majina ya watu hao watatu yamehifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi mzima wa tukio hilo la kinyama.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post