WAHANDISI 630 KULA KIAPO CHA UTII MAADHIMISHO SIKU YA WAHANDISI 2021


Na Dotto Kwilasa - Dodoma

Jumla ya Wahandisi  wataalamu 630, wanatarajia kula kiapo cha utii wa taaluma yao kitakachotumiwa na vyombo mbalimbali kuwawajibisha pale watakapokiuka sheria na taratibu katika majukumu yao ya kiutendaji.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mkutano mkuu 18 wa Bodi ya Usajili Wahandisi nchini (ERB) Prof, Bakari Mwinyiwiwa, wakati  akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya Wahandisi Tanzania mwaka 2021.

Amesema kiapo hicho kitawaandaa Wahandisi hao na kuhakikisha kuwa wanawajibika vyema katika taaluma zao,maamuzi pamoja na utendaji wao wa kihandisi wa kila siku.

 "Maadhimisho hayo yamepangwa kufanyika jijini hapa, kwa siku mbili kuanzia Septemba 2  na 3, 2021 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete. Pamoja na mambo mengine katika maadhimisho hayo jumla ya Wahandisi 630, watakula kiapo ya utii wa taaluma yao ili kuwafanya wawajibike katika utendaji wa mambo mbalimbali kwenye taaluma yao,"amesema 

"Bodi ilianzisha utaratibu wa wahandisi wataalamu wote kula kiapo cha utii kwa taaluma yao na kwamba itakuwa ni mwiko kwao kukiuka miiko ya taaluma ya uhandisi",ameongeza  Prof. Mwinyiwiwa

Amefafanua kuwa maudhui ya kiapo hicho yatakuwa ni wahandisi kuanza kuitumikia taaluma kama mtaalamu, kiapo kitamkumbusha jukumu lake kitaalamu na umuhimu wa kuzingatia taaluma wakati wote.

Amesema kiapo kitaufanya umma ujenge imani kwa Wahandisi husika kitatumika dhidi ya muhandisi atakapo vunja miiko na maadili ya taaluma katika kumchukulia hatua Mhandisi atake kiuka kiapo chake.

"Kiapo kitamlinda Mhandisi dhidi ya kulazimishwa kutenda mambo ambayo ni kinyume na taaluma yake,pia kitamkumbusha kuzingatia thamani ya fedha,usalama wa maisha ya binadamu na mazingira,kutoruhusu masuala ya jinai,kidini,jinsia,ukabila,rangi,milengoya kisiasa katika kutekeleza kazi zake za uhandisi", amesisitiza Prof. Mwinyiwiwa

Amesema katika majadiliano kitaaluma mada kuu itakuwa ni athari za mapinduzi ya nne ya viwanda kwenye miundombinu na viwanda kwa uendelevu wa uchumi wa kati.

"Pia zitakuwepo mada ndogo kamavile mafunzo na kujenga uwezo,miundombinu na maendeleo ya viwanda, namna na mbinu za kuhimili msongo wa mawazao kwa afya njema",alisema Prof. Mwinyiwiwa.

Kadhalika alisema katika maadhimisho hayo kutakuwa na zoezi utoaji wa tuzo kwa Wahandisi na wahitimu wa taasisi.

"Hii ni moja ya shughuli kubwa itakayofanyika wakati wa kuadhimisha siku ya wahandisi kwa mwaka huu bodi itatoa tuzo kwa makundi ya wahandisi wahitimu kutoka vyuo vikuu na taasisi za uhandisi nchini mwaka 2019/20",amesema

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments