Maajabu !! SAMAKI MWENYE KICHWA CHA KONDOO NA MENO YA BINADAMU APATIKANASamaki mwenye kichwa cha kondoo na meno ya binadamu
Samaki asiye wa kawaida mwenye meno ya binadamu amekamatwa nchini Marekani.

Picha ya samaki huyo ilisambazwa katika mtandao wa facebook .

Alitambuliwa kama samaki mwenye kichwa cha kondoo 'Sheephead fish', ambaye ana meno kama ya binadamu ya kuvunja chakula.

Samaki huyo anaonekana kupata jina hilo kutokana na mdomo wake kuwa na muonekano kama ule wa kondoo.

Samaki huyo anadaiwa alikamatwa na Nathan Martin ambaye amekuwa katika gati hiyo.

Bwana Martin alisema alikuwa na matumaini ya kumshika samaki mwenye kichwa cha kondoo wakati alipoona mdomo uliojaa meno.

Chanzo - BBC Swahili

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post