ASKOFU GWAJIMA : SIJALISHWA SUMU NA HAITATOKEA - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Sunday, August 8, 2021

ASKOFU GWAJIMA : SIJALISHWA SUMU NA HAITATOKEA

Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima mbaye pia ni mbunge wa jimbo la Kawe jijini Dar es salaam amekanusha madai kuwa amelishwa sumu kutokana na msimamo wake kuhusu chanjo ya UVIKO -19.

Akizungumza leo Jumapili Agosti 8, 2021 wakati wa ibada kanisani kwake kuwa hajalishwa sumu nahakuna wa kumnywesha sumu na hatotokea.

"Wanataka kusingizia watu, labda kusingizia kwamba serikali imeninywesha sumu. Niwahakikishie kwamba hakuna serikali imemnywesha sumu Gwajima kwa kuwa serikali ndiyo inasema chanjo ni hiari. Suala la afya ya mtu linapaswa kulindwa na mtu mwenyewe. Labda nitoe changamoto kwa wanaojiita watalaam waje walete andiko linaloonyesha kemikali zilizopo kwenye chanjo", amesema Gwajima.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages