RC SENGATI AZINDUA CHANJO YA CORONA SHINYANGA...MGEJA ASEMA WANAOPOTOSHA NI MAGAIDI WASHUGHULIKIWE


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akipata chanjo dhidi ya UVIKO - 19  wakati akizindua Chanjo dhidi ya UVIKO - 19 mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Agosti 4,2021
**
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizungumza leo Jumatano Agosti 4,2021 wakati akizindua Chanjo dhidi ya UVIKO - 19 mkoa wa Shinyanga amesema Chanjo hiyo inatolewa kwa lengo la mwili kutengeneza kinga dhidi ya janga la Corona.

Amesema Chanjo dhidi ya UVIKO - 19 ni salama hivyo kuwasihi wananchi walio tayari kuchanjwa wajitokeze kuchanjwa huku akiwataka kuwapuuza wanaopinga chanjo hiyo.

"Leo katika mkoa wa Shinyanga tunaanza rasmi utoaji chanji dhidi ya UVIKO - 19. Kwa awamu ya kwanza tumepokea dozi 25,000 za chanjo katika mkoa wa Shinyanga ambazo zitatolewa katika vituo 18 kwenye mkoa. Chanjo hii itasaidia kupunguza kasi ya maambukizi ya Virusi vya Corona hivyo nawaomba wananchi wajitokeze kupata chanjo hii ambayo inatolewa bure kwa wananchi ambao wapo tayari kuchanjwa",amesema Dkt. Sengati.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taasisi ya Mzalendo Foundation ambaye pia ni Mwenyekiti Mstaafu wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akizungumza baada ya kupata chanjo ya UVIKO - 19 ameiomba serikali kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaopotosha kuhusu Chanjo ya COVID - 19 akisema hao ni sawa na magaidi.

"Hawa wanaopotosha kuhusu Chanjo ya UVIKO - 19 ni magaidi. Upotoshaji huu ni aina mpya ya Ugaidi wachukuliwe kama wahalifu wengine. Kama unazuia watu wasichanjwe maana yake unataka wafe, kwa hiyo hawa ni sawa na magaidi",amesema Mgeja.

"Wanaopotosha dhidi ya Chanjo ya UVIKO - 19  wachukuliwe kama wahalifu wengine. Hawa ni sawa na wauaji wa Kimbari. Wachukuliwe hatua za kisheria, tusiwachekee kwani ukicheka na Nyani utavuna mabua",amesema Mgeja.

Ameeleza kuwa Taaluma ya Kitaalamu inakosolewa kitaalamu siyo kuingiza siasa na upotoshaji hivyo wanaopinga chanjo ya UVIKO - 19 ni bora wakae kimya au watupe mbadala wa chanjo badala ya kupotosha tu.

"Ninampongeza Mhe. Rais Samia Suluhu kwa kukubali Watanzania wapatiwe chanjo dhidi ya UVIKO - 19 na Mkuu wetu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati kuhamasisha wananchi wapate chanjo, nami nimejitokeza kuwa miongoni mwa Watanzania wa mwanzo kabisa kuchanjwa chanjo dhidi ya UVIKO - 19. Naomba wananchi wajitokeze kuchanjwa....Akili za kuambiwa changanya na zako, wawapuuze hao wapotoshaji, hao magaidi",ameongeza Mgeja.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizungumza wakati akizindua Chanjo dhidi ya UVIKO - 19 mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Agosti 4,2021 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizungumza wakati akizindua Chanjo dhidi ya UVIKO - 19 mkoa wa Shinyanga
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile akizungumza wakati wa uzinduzi wa  Chanjo dhidi ya UVIKO - 19 mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Agosti 4,2021 
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary akizungumza wakati wa uzinduzi wa  Chanjo dhidi ya UVIKO - 19 mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Agosti 4,2021.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akisaini Fomu ya Uhiari wa kupata chanjo dhidi ya UVIKO - 19  wakati akizindua Chanjo dhidi ya UVIKO - 19 mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Agosti 4,2021
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akipata chanjo dhidi ya UVIKO - 19  wakati akizindua Chanjo dhidi ya UVIKO - 19 mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Agosti 4,2021
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akipata chanjo dhidi ya UVIKO - 19  wakati akizindua Chanjo dhidi ya UVIKO - 19 mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Agosti 4,2021
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mzalendo Foundation ambaye pia ni Mwenyekiti Mstaafu wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akipata chanjo dhidi ya UVIKO - 19  wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizindua Chanjo dhidi ya UVIKO - 19 mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Agosti 4,2021
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mzalendo Foundation ambaye pia ni Mwenyekiti Mstaafu wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akizungumza baada ya kupata chanjo dhidi ya UVIKO - 19  wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizindua Chanjo dhidi ya UVIKO - 19 mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Agosti 4,2021
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akipata chanjo dhidi ya UVIKO - 19  wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizindua Chanjo dhidi ya UVIKO - 19 mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Agosti 4,2021
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akipata chanjo dhidi ya UVIKO - 19  wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizindua Chanjo dhidi ya UVIKO - 19 mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Agosti 4,2021
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando akipata chanjo dhidi ya UVIKO - 19  wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizindua Chanjo dhidi ya UVIKO - 19 mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Agosti 4,2021
Mkurugenzi wa Malunde 1 blog / Mwandishi wa Habari/ Blogger, Kadama Malunde akipata chanjo dhidi ya UVIKO - 19  wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizindua Chanjo dhidi ya UVIKO - 19 mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Agosti 4,2021
Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga Sheikh Hamis Balilusa akipata chanjo dhidi ya UVIKO - 19  wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizindua Chanjo dhidi ya UVIKO - 19 mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Agosti 4,2021
Mkurugenzi wa Karena Hotel,Josephine Wambura akipata chanjo dhidi ya UVIKO - 19 wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizindua Chanjo dhidi ya UVIKO - 19 mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Agosti 4,2021
Mwandishi wa Habari, Marco Mipawa akipata chanjo dhidi ya UVIKO - 19  wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizindua Chanjo dhidi ya UVIKO - 19 mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Agosti 4,2021
Mwandishi wa Habari, Shaban Alley akipata chanjo dhidi ya UVIKO - 19  wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizindua Chanjo dhidi ya UVIKO - 19 mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Agosti 4,2021
Dkt. Danny Mzee akipata chanjo dhidi ya UVIKO - 19  wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizindua Chanjo dhidi ya UVIKO - 19 mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Agosti 4,2021
Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, Joseph Paul akipata chanjo dhidi ya UVIKO - 19  wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizindua Chanjo dhidi ya UVIKO - 19 mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Agosti 4,2021
Wadau wakifuatilia matukio wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizindua Chanjo dhidi ya UVIKO - 19 mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Agosti 4,2021
Wadau wakifuatilia matukio wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizindua Chanjo dhidi ya UVIKO - 19 mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Agosti 4,2021

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post