CHADEMA SHINYANGA WAENDESHA MAOMBI MAALUM KUMUOMBEA MBOWE

 


Wanachadema Jimbo la Shinyanga Mjini wakiwa katika maombi ya kumuombea Mwenyekiti wao wa Taifa Freeman Mbowe na wenzake ambao wapo Mahabusu.


Na Marco Maduhu, Shinyanga


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Shinyanga Mjini, kimeendesha maombi maalum ya kumuombea Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Freeman Mbowe pamoja na wenzake, ambao wapo mahabusu wakikabiliwa na tuhuma mbalimbali zikiwemo za ugaidi na uhujumu uchumi.


Maombi hayo yamefanyika leo kwenye Ofisi cha Chadema Kanda ya Serengeti Mjini Shinyanga  yakiongozwa na Mchungaji Mussa Kagoma kutoka Kanisa la Matengenezo.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa maombi hayo,Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Shinyanga Mjini Hamis Ngunila amewataka wanachadema waendelee kusimama imara licha ya kukabiliwa changamoto mbalimbali za kisiasa, ikiwemo kukamatwa viongozi wao wa ngazi za juu.

“Ndugu zangu misukosuko ambayo wanapitia viongozi wetu, ni njia ya kutudhoofisha, na kututoa kwenye njia ya kudai Katiba Mpya, hivyo tusikate tamaa tuendelee kusimama imara na kukipigania chama,”amesema Ngunila.

“Chadema jimbo la Shinyanga mjini tumejipanga kufanya makongamano ya kudai Katiba Mpya kwenye kata zote 17 za mjini Shinyanga, na Katiba ndiyo itakuwa salama kwetu sisi na watanzania wote hasa kwenye suala la kupatikana kwa haki,”ameongeza Ngunila.

Naye  Katibu wa Baraza la wanawake mkoa wa Shinyanga (BAWACHA) Agatha Mamuya, amewataka wanachadema kusimama imara pamoja na Mwenyekiti wao Taifa Freeman Mbowe, na kumuombea dhidi ya kesi ambazo zinamkabili ashinde na kuachiwa huru

Kwa upande wake Mchungaji wa Kanisa la Matengenezo la Mjini Shinyanga Mtume Mussa Kagoma, akizungumza kabla ya kuendesha maombi, amewataka viongozi wawe waumini wa kutenda haki, ili kuendelea kudumisha amani ya nchi.


Mchungaji wa Kanisa la Matengenezo Shinyanga Mjini Mtume Mussa Kagoma, akiongoza maombi ya kumuombea Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe.

Maombi yakiendelea.

Maombi yakiendelea.

Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Shinyanga Mjini Hamis Ngunila, akizungumza na Wanachadema, mara baada ya maombi kumalizika.

Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Shinyanga Mjini Hamis Ngunila, akiendelea kuzungumza na Wanachadema wa Jimbo hilo.

Katibu wa Baraza la Wanawake Chadema BAWACHA Mkoa wa Shinyanga Agatha Mamuya, akizungumza na Wanachadema, mara baada ya kumalizika kwa maombi maalum ya kumuombea Mbowe.

Wanachadema wakiwa kwenye maombi maalum ya kumuombea Mbowe, pamoja na kusikiza Nasaha za viongozi wao.

Wanachadema wakiwa kwenye maombi maalum ya kumuombea Mbowe, pamoja na kusikiza Nasaha za viongozi wao.

Wanachadema wakiwa kwenye maombi maalum ya kumuombea Mbowe, pamoja na kusikiza nasaha za viongozi wao.

Wanachadema wakiwa kwenye maombezi maalum ya kumuombea Mbowe, pamoja na kusikiza Nasaha za viongozi wao.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post